Alhaj Dk. Mwinyi
amewatembelea Bw. Haji Ramadhan Suweid Buda, mwandishi wa habari mkongwe na
mama mzazi wa Sheikh Samir Zulfikar wa Mahad el Juneid ya Mkunazini ambao
wanaendelea na matibabu hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Pia Alhaj Dk. Mwinyi
aliwatembelea wazee wa Chama cha Mapinduzi ambao walitoa mchango mkubwa kwenye
chama hicho akiwemo Bw. Kombo Mzee Kombo nyumbani kwake Miembeni Mkoa wa mjini
Magharibi, Bw. Bora Afya Silima Haji nyumbani aliekua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Mjini Kichama nyumbani kwake Mwembelikunda na bi. Hiari Miraji Othman, Balozi
wa nyumba 10 namba mbili huko nyumbani kwake Miembeni jitini.
Mapema, Alhaj Rais
Dk. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislam na wananchi wa Miembeni
kwenye ibada ya sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Ijumaa, Miembeni, Wilaya ya
Mjini.
Akizungumza kwenye
ibada hiyo Katibu Mtendaji
kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwahimiza waumini wa
Kiislam umuhimu wa tabia njema na kueleza kuwa tabia njema ni msingi wa mambo
manne ikiwemo imani.
Sheikh Khalid alieleza kwenye tabia njema
imani hudumu kwa kutekelezwa amri za Allah (S.W) pamoja na kufuatwa makatazo
yake. Pia alieleza kukosekana kwa tabia njema imani hupungua na kuongezeka kwa vitendo
vya kuporomoka kwa maadili ikiwemo kupungua kwa heshima kwenye familia na
jamii.
Alisema siku hizi watoto hawawaheshimu wakubwa
zao wakiwemo wazazi na walezi hata jamii zinazowazunguruka, aliiasa jamii ili
kupunguza wimbi la ukosefu wa maadili na kuepusha athari kubwa za ndoa na
takala zinazojitokeza kwenye jamii ni vyema kutafuta njia za busara ili kukinusuru
kizazi cha sasa kilichogubigwa na wimbi la ukosefu wa heshima na maadili.
Pia aliiasa jamii kuendelea kuwafundisha
mema watoto ili kukuza jamii yenye heshima na maadili mema na tabia njema.
Kwa upande wake, Khatib
wa ibada hiyo ya sala ya Ijumaa aliiasa
jamii kwamba uzuri wa waumini na waislam ni elimu, adabu na kuheshimu viongozi na
jamii inayowazunguruka kwa kujiepuka kutoa maneno yasiyofaa kwa viongozi, wazazi
na jamii ili kujenga jamii iliyonjema.
IDARA YA MAWASILIANO,
IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment