Habari za Punde

Tamasha la michezo kimataifa kufanyika Zanzibar mwakani

Mwenyekiti wa Tamasha la michezo la kitaifa ZISF Mohammed Salim Mohammed akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kuanza February 08, 2024. 

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu Tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kuanza February 08, 2024.


 PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

Na Fauzia Mussa,       Maelezo

 

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amewataka wadau wa michezo  kubuni matamasha ya michezo ya kimataifa  ili  kuvutia watalii.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uwepo wa tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kufanyika mwaka 2024  amesema kuzinduliwa kwa Tamasha hilo litakaloshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo tennis  kutasaidia Vijana kuonyesha vipaji vyao kimataifa.

 

Amesema Zanzibar kuna vipaji vingi vya michezo hivyo uwepo wa  Tamasha hilo kutawawezesha vijana kupata fursa ya kujitangaza kimataifa .

 

Aidha alisema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya michezo ikiwemo kujenga viwanja vyenye ubora ili kuweza kukidhi hadhi za kimataifa

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tamasha la michezo la kitaifa ZISF Mohammed Salim Mohammed amesema Tamasha hilo lina lengo la kukuza na kuongeza fursa za uwekezaji wa utalii wa  michezo ambao utalenga kuiweka Zanzibar kuwa kivutio cha utalii Duniani kote.

 

Amesema Tamasha la uwekezaji wa utalii wa michezo linatarajiwa Kufunguliwa  Februari  08 hadi 12,2024  ambapo litajumuisha Mchezo wa baskel ,marathon ,soka ya ufukweni na tenis ya kimataifa na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbali mbali za Afrika na nje ya Afrika.

 

"Katika Tamasha hili tunarajia kushirikisha Wana michezo kutoka  Kenya, Uganda, Tanzania , Burundi Rwanda, Sudani ya Kusini ,Kongo, Afrika Kusini, Moroko, Misri, Algeria, Ethiopia, Zambia, Malawi,Zimbabwe na Namibia na washiriki kutoka nje ya Afrika ikiwemo   Polandi,Uiengereza,Ujerumani Italia Ufaransa na Marekani." Alifahamisha Mwenyekiti ZSFI

 

Nae Mkurugenzi wa masoko kamisheni ya utalii Rahma sanya amesema  wanaendelea kuuwaunga mkono wadau wa  Michezo ya kimataifa kwani michezo  hiyo ni miongoni mwa  Sababu ya kuwarejesha watalii Zanzibar baada yamuda mrefu  kuzowea kuja kutalii fukwe,bahari na Hali ya hewa nzuri iliopo nchini.

 

Hatahivyo amesema jukumu la kuutangaza utalii ni la kila mmoja  hivyo Wizara inawakaribisha wadau hao ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika  kuitangaza Zanzibar Duniani kote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.