Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Akilifungua Jengo la Ofisi ya KMKM Mkoa wa Kusini Unguja Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la  ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Utawala KMKM Kamandi ya Mkoa wa Kusini Unguja, eneo la Unguja Ukuu, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akikata utepe kulifungua  Jengo la Ofisi ya Utawala KMKM Kamandi ya Kusini Unguja Unguja Ukuu, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuweka mazingira mazuri  kwa maafisa na wapiganaji wa vikosi vya ulinzi na usalama ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kufikia malengo ya mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua jengo la ofisi ya Utawala la KMKM Kamandi ya kusini Unguja eneo la UNGUJA UKUU  Wilaya ya Kati  ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu iliyoimara kwa vikosi vya ulinzi na usalama ikiwemo kikosi cha Maalum cha kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) ikiwa ndio azma ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya kuimarisha vikosi vya Ulinzi ili kuendana na mabadiliko yanayojitokeza ulimwenguni pamoja na kuwajengea uwezo na utayari wa ulinzi kwa raia na mali zao.

Mhe. Hemed amesema  dhana ya mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 ni kuwaletea maendeleo wananchi wake  bila ya ubaguzi wa aina yoyote pamoja nakuimarisha ulinzi wa nchi pamoja na raia na  mali zao  pamoja na kuimarisha taasisi mbali mbali za kiserikali ili kuwarahisishia wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

Makamu wa pili wa Rais amekitaka kikosi cha KMKM  kulitunza jingo hili ili liweze kutumika kama lilivyokusudiwa na serikali pia amesema ni vyema Viongozi kuwajibika na kutenda haki kwa kulinda raia na mali zao na kuhakikisha inapambana na wale wote wanaohujumu uchumi kwa kusafirisha bidhaa kwa njia ya magendo jambo ambalo linaleta madhara kwa serikali pamoja na kurejesha maendeleo nyuma.

Sambamba na hayo  Mhe. Hemed amevipongeza vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini pamoja na kuonesha utayari wao wa kujenga miradi ya kimaendeleo ambayo inaisaidia serikali kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Nae  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi Maalum vya SMZ Ndugu Issa Mahfoudh Haji amesema Mradi wa Ujenzi wa ofisi ya kikosi cha kuzuia magendo Kamandi ya kusini ni muendelezo wa ujenzi wa majengo ya ofisi, Nyumba na Mahanga kwa wapiganaji ikiwa na leongo la kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili askari na maafisa wa KMKM kwa unguja na Pemba.

Amesema kuwa kukamilika kwa Ofisi hii italeta  mapinduizi  makubwa pamoja na  kuwapunguzia changamoto za ofisi lwa Maafisa na Akari wa kikosi cha KMKM ambapo Mradi ambapo umetumia zaidi ya shilingi  Bilioni  1.1  zimetumika kwa  usambazaji wa vifaa ambapo mafundi na vibaruawa mradi huko ni askari na maafisa wa kikosi hicho.

Mapema Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja  Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka askari na maafisa wa Kikosi cha kuzuia magendo KMKM kufanya kazi kwa uangalifu wa hali ya juu pamoja na kuhakikisha wanapambana na wale wote ambao wanasafirisha magendo kitendo ambacho hurejesha nyuma maendeleo ya serikali.

Amesema kuwa Kamadi ya kusini inakabiliwa na sehemu kubwa na habari ambayo inabandari zisizokuwa rasmi hivyo ni wajibu wa kila askari na afisa kutimiza wajibu wake katika ulizi na usalama wanchi hii.

Mkuu wa Kikosi Maalum  cha kuzuia Magendo Zanzibar  KMK M  Komodoo Azana Hassan Msingiri amemuhakikishia Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar kuwa jingo hili la Kmandi ya Kusini limejengwa na askari na maafisa wa KMKM kwa lengo la kuisaidia serikali katika kujenga majengo ya kisasa ambayo yatawaondolea wapiganaji changamoto za ofisi.

Msingiri amesema kuwa jingo limekamilika kwa asilimia mia moja lakini bado linakabiliwa na changamoto ya fanicha hivyo ameiomba serikali kuwatatulia changamoto hio ili kuleta ufanisi nzuri wa kazi kwa maafisa na wapiganaji wa kikosi hicho.

Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR)

Leo tarehe..30.12.2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.