RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amezuru kaburi la Rais Mstaafu wa Zanzibar Marehemu Sheikh Idrissa Abdulwakil na kujumuika na Viongozi na Familia ya
Marehemu kumuombea dua iliyosomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,
iliyofanyika katika kaburi la marehemu Kijijini kwao Makunduchi, wakati wa
ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuria dua maalum ya kuwaombea
Viongozi Wakuu na kuiombea Nchi Amani, dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti
Mkuu wa Ijumaa Mtegani Makunduchi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Katiba,Sheria.Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na
(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Galos Nyimbo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Familia ya
Marehemu Sheikh Hassan Bin Ameir, alipofika katika kaburi la marehemu katika
Kijiji cha Mtegani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, kwa ajili ya kumombea
dua ,akiwa katika ziara yake na
kuhudhuria dua maalum ya kuwaombea
Viongozi Wakuu wa Nchi na kuiombea Nchi Amani,iliyofanyika katika msikiti Mkuu
wa Ijuma Mtegani Makunduchi leo 16-12-2023.
No comments:
Post a Comment