Habari za Punde

BALOZI SEIF ATAKA MAONESHO YA KAZI ZINAZOFANYWA NA TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI KUENDELEZWA

Makamu wa pili wa Rais mstaafu Balozi Seif Ali Iddi  akipokea maonesho ya kazi zinazofanywa na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi kupitia magari yaliyoandaliwa na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais kazi Uchumi na uwekezaji ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Na Rahma Khamis Maelezo     4/1/2024

Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi ameitaka Wizara ya Nchi (OR),kazi uchumi na uwekezaji  kuendelea kufanya maonesho ya kazi zinazofanya na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ili kutoa fursa kwa wanachi kuweza kutambua kazi hizo.

Ameyasema hayo huko Kisonge Mnara wa Kumbukumbu mara baada ya kupokea maonesho hayo kupitia magari  ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 Mapinduzi yalioasisiwa  mwaka 1964.

Amesema iwapo maonesho hayo yataendelezwa na kudumishwa yatasaidia taasisi hizo kutangaza kazi zao pamoja na kukuza uchumi wa nchi, kuleta maendeleo sambamba na kuinua kipato cha mtu mmojammoja  na taifa kwa ujumla.

“Iwapo maonesho haya yataendelezwa kufanywa kila mwaka basi yataimarisha biashara za wananchi na mambo  yataendelea kuwa mazuri”alisema Balozi Seif.

Awali alisema maonesho kama hayo yalifanyika miaka 10 nyuma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi hivyo ipo haja ya wizara husika kushirikiana na taasisi hizo kuyaendeleza ili kuleta tija kwao na wananchi kwa ujumla .

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi ,Uchumi na Uwekezaji Mhe, Mudrik Ramadhan Soraga amesema kuwa Wizara imeona ipo haja kushajihisha taasisi hizo kujitangaza ili wananchi waweze kufahamu kwa namna gani wataweza kupata huduma zinazotolewa na  taasisi zao.

Amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kuwapa mwamko mpana zaidi wananchi  kujituma ili iwe ni chachu ya kujenga taifa na kuakiasi malengo ya waasisi katika kuona misingi na heshima ya utu ipo katika kufanya kazi.

Aidha amefahamisha kuwa kupitia maonesho hayo wamejenga  ushirikiano mkubwa na kubadilishana uzoefu  kati ya  taasisi zilizoshiriki maonesho hayo yaliyofanyika kupitia magari.

“tumeona taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimeshiriki katika maonesha haya na wamepata nafasi ya kuonesha kazi zao  kwa wananchi hivyo kwa muamko tuliyouona leo tunarajia kufanya maonesho mengine kama hayo ifikapo Mei mosi ili kutoa fursa kwa watendaji na wananchi kushiriki maonesho hayo.”alisema Mhe.Soraga.

Nao baadhi ya washiriki wa  maonesho hayo akiwemo Amina said Ali  amesema kuwa wamefurahishwa na mfumo huo kwani kupitia maonesho hayo wameweza kujitangaza na kuuza bidhaa zao.

Aidha ameiomba wizara husika kuandaa maonesho hayo mara kwa mara ili kupata fursa ya kuijatangaza.

Maonesho hayo kupitia magari yalianzia Maisara na kupokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu ya mapinduzi  Kisonge na kumalizikai Viwanja vya Maisra ambapo taaisi zilizoshiriki zilipata fursa ya kutangaza huduma zinazopatikana katika taasisi zao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.