Habari za Punde

WAZIRI MAKAMBA KUMWAKILISHA MHE RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA NNE WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA ITALIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Italia.Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, alipowasili Roma Italia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassankatika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaotarajiwa kufanyika 28 na 29 , Januari 2024. Roma, Italia.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Italia Mhe.Mahmoud Thabit Kombo , alipowasili Roma, Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 - 29 Januari 2024, Roma, Italia. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), amewasili Roma, Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 - 29 Januari 2024, Roma, Italia.                                                                                                    

Mara baada ya kuwasili, Waziri Makamba amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mohmoud Thabit Kombo.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo wa wangazi ya Wakuu wa Nchi wa Afrika na Italia, unatarajiwa kujadili ajenda mbalimbali zikijumuisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu, ushirikishwaji wa wahamiaji katika kuleta maendeleo, usalama wa chakula, mapambano dhidi ya ugaidi na matumizi ya teknolojia ya kidigitali.

Ajenda nyingine ni pamoja na uhamiaji haramu, mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, mabadiliko ya tabianchi, ushirikiano katika sekta ya elimu kupitia ngazi ya vyuo vikuu na katika mafunzo ya ufundi na utamaduni.

Kupitia mkutano huo Serikali ya Italia inatarajia kujipambanua kama mshirika muhimu wa maendeleo wa bara la Afrika kupitia mpango mpya wa maendeleo utakaotambulishwa kwa mara ya kwanza uitwao Mattei Plan. Mpango huo unalenga kuifanya Italia kushirikiana kwa karibu na bara la Afrika katika nyanja za maendeleo ya usawa na unatarajiwa kutambulishwa kwa nchi zingine za Umoja wa Ulaya hapo baadae utakapoanza utekelezaji.  Vilevile kupitia Mkutano huo Italia inatarajia kutangaza kuunga mkono umuhimu wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) kuwa mwanachama kwenye Kundi la G-20. 

Kadhalika, Italia inatarajia kutumia fursa ya mkutano huo, kuonesha utayari wake wa kuhamisha teknolojia ya kisasa (the know-how) katika sekta ya kilimo kwa nchi za Afrika na kuwa kitovu cha usambazaji wa Nishati kutoka Bara la Afrika.

  

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.