Habari za Punde

Katibu Mkuu Bi Fatma Wataka Watendaji Wizara ya Habari Kuacha Kufanya Kazi Kwa Tamaa

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo.Bi. Fatma Hamad Rajab amewataka watendaji wa wizara ya habari kuwacha kufanya kazi kwa tamaa ili kuimarisha maendeleo na kufikia kwa malengo yanayotakiwa.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo  ya watendaji wa  miradi yaliyowashirikisha wajumbe wa bodi ya zabuni ya wizara, wakiwemo maafisa manunuzi, wanasheria na maafisa mipango.

Amesema iwapo watendaji hao watafanya kazi kwa pamoja na kuondosha taamaa wataweza kufata nyayo za viongozi na kufikia hatuwa zinazotakiwa.

Afisa ujengaji uwezo na huduma za ushauri kutoka mamlaka ya ununuzi na uondoaji wa mali za umma Hafidh Rashid Zam amesema kutofata sheria, kanuni na miongozo ya manunuzi kutasababisha kutofikia malengo ya serikali ambayo imejipangia.

Ameeleza kuwa mamlaka ya ununuzi ndio taasisi iliyopewa jukumu kisheria kushuhulikia taratibu zote za kimanunuzi kwa fedha za mali za umma.

Nae kaimu mkurugenzi mipango sera na utafiti kutoka wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo nd.  Omar Juma Ali amesema lengo la kikao hicho ni kuwajengea uwezo watendaji  katika suala zima la usimamizi wa miradi na udhibiti kutokana na kujitokeza kwa matatizo katika kusimamia  miradi.

Ameongeza kuwa mwaka wa fedha 2024-2025 watahakikisha wanazifanyia kazi na kuondosha kasoro zote zilizojitokeza kipindi cha nyuma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.