Habari za Punde

Oman na Tanzania Zakabidhiana Vifaa vya Uhifadhi wa Mikusanyo ya Kimakumbusho

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akishuhudia makabidhiano ya vifaa vya awali kati ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho ya Sultani ya Oman, vitakavyotumika kwa ajili ya kuhifadhia mikusanyo mbalimbali iliyopo katika  Makumbusho ya Tanzania leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe.  Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga (kulia) vifaa vya awali vya kuhifadhia mikusanyo mbalimbali katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akionyeshwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe.  Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) eneo la Maktaba ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania lililotengwa maalum kwa ajili ya machapisho ya Oman.
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe.  Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)miongoni mwa mikusanyo ya picha itakayokuja kuwekwa kwenye ukumbi mpya wa kudumu wa kihistoria, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa.

Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe.  Jamal bin Hassan Al Moosawi  (hayupo pichani) katika kikao na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shaidhani.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shaidhani (kulia), Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe.  Jamal bin Hassan Al Moosawi(wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga(wa tatu kutoka kushoto), Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni , Adelaide Salema (wa pili kutoka kulia) na Mshauri wa Masuala ya Historian na Utamaduni Oman Abdulwahab Al Busaidi (kushoto) mara baada ya kikao cha wataalamu kati ya  Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.