Habari za Punde

Benki ya CRDB Kushirikiana na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Katika Nyanja Mbalimbali za Huduma za Kifedha

 

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zubeir Ali Maulid,amesema, benki ya CRCB imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na baraza la wawakilishi katika nyanja mbalimbali katika huduma zankifedha na hata katika michezo.

Spika Zubeir, ameyasema hayo alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya elimu ya fedha na huduma za kifedha zitolewazo na benki ya CRDB kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa baraza hilo Chukwani Mjini Unguja.

Amesema, benki ya CRDB ni benki ambayo kila siku imekuwa inaleta ubunifu mkubwa katika utoaji wa huduma za kifedha nchini hivyo, ameipongeza benki hiyo kwa jitihada hizo nzuri ambazo zinaunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha watanzania walio wengi wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa kifedha kwa kutoa mafunzo mbalimbali juu ya elimu ya fedha.

"Ni kweli ulio wazi kuwa sekta ya fedha inq mchango mkubwa sana katika ukuaji na maendeleo ya uchumi, kujenga uchumi jumuishi na kupunguza umasikini" amesema.

Hivyo, amesema duniani kote serikali zimekuwa zikitilia mkazo suala la elimu ya fedha ili kuleta ujumuishi katika huduma za fedha sambamba na hatua mbalimbali za kisera ili kukuza ujumuishi wa fedha kwa wananchi.

Hivyo, amewataka wajumbe wa baraza hilo kuyatumia vizuri mafunzo hayo katika kujiongexea maarifa binafsi sambamba na kuleta weledi katika kutimiza majukumu ya uwakilishi wa wananchi.

Akizungunza kwa niaba ya mkurugenzi wa benki hiyo,Afisa Mkuu wa Biashara CRDB,Boma Raballa, alisema, wataendelea kufanya kazi na watendaji wa baraza hilo ili lengo liweze kufikiwa.

Amesema benki hiyo imekuwa ikitoa zabuni na dhamana yabutendaji, dhamana ya malipo ya malipo pamoja na punguzo la Ankara sambamba na ufadhili wa agizo la ununuzi  wa vitu mbalimbali.

Katibu wa Baraza la wawakilishi, Raya Issa Mselem, amesema wanafarijika sana kuwa na ushirikiano na benki hiyo sambamba na  kufurahia huduma wanazozitoa benki hiyo kwani wamekuwa wakifanya kazi zao kwa wakati.

Hata hivyo, alipongeza benki hiyo kwa kuwapa semina hiyo na kuahidi kuendelea kuwa nao katika utoaji wa huduma zilizokuwa bora zaidi.

Wakichangia wajumbe hao, wamesema benki hiyo imekuwa mchango mkubwa katika kuhakikisha miradi wanayoyaanzisha yanaendelea kuimarika.

Hata hivyo, wajumbe hao wameipongeza benki hiyo kwa huduma zao nzuri wanazozitoa katika utoaji huduma mbalimbali za kifedha.
Mkurugenzi wa Benki  hiyo,Afisa Mkuu wa Biashara CRDB,Boma Raballa, alisema, wataendelea kufanya kazi na watendaji wa baraza hilo ili lengo liweze kufikiwa.
Afisa Mkuu wa Biashara CRDB,Boma Raballa, alisema, wataendelea kufanya kazi na watendaji wa baraza hilo ili lengo liweze kufikiwa.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.