Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Aipongeza TIGOZANTEL Kuboresha Uboreshaji wa Huduma za Mawasiliano



Afisa Mkuu wa Fedha kutoka TigoZantel CPA. Innoent Rwetabura amesema kampuni yao imekua ikifanya juhudi mbalimbali katika kuboresha mawasiliano nchini ambapo kwa kutambua juhudi hizo kampuni yao imepata nafasi ya kuthibitishwa kuwa mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania mwaka 2023/2024 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla 

ameipongeza kampuni hiyo kwa kufanikisha uwekaji wa miundombinu ambayo imewezesha upatikanaji wa mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa asilimia tisini na saba

Mheshimiwa Hemed ametoa pongezi hizo wakati alipojumuika na wananchi mbalimbali katika iftar iliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo Zantel na kuanyika katika hotel ya golden tulip Airport Zanzibar

Amesema miradi mikubwa inayofanywa na kampuni hiyo ya kufunga minara imewezesha kuboresha upatikanaji wa  mawasiliano katika maeneo yote ya Unguja na Pemba

Amesema awali kulikua na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano jambo ambalo lilipelekea kuzorota kwa shughuli mbalimbali za kijamii na uchumi

Katika hatua nyengine ameitaka kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo zantel kushirikiana na mamlaka nyengine katika kudhibiti matukio ya kiuhalifu pamoja na udnaganyifu yanayofanywa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya simu

Amesema matukio ya udanganyifu kwenye mitandao ya simu yanapaswa kudibitiwa kwa kuhakikisha wanawafatilia wafanyaji wa matukio hayo ili kuchukuliwa hatua za kisheria

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Fedha kutoka TigoZantel CPA. Innoent Rwetabura amesema kampuni yao imekua ikifanya juhudi mbalimbali katika kuboresha mawasiliano nchini ambapo kwa kutambua juhudi hizo kampuni yao imepata nafasi ya kuthibitishwa kuwa mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania mwaka 2023/2024 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.