Habari za Punde

DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA OXFORD POLICY MANAGEMENT

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Wataalam kutoka Oxford Policy Management Ofisini kwake.

Mratibu wa Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya 

Awali ya Mtoto kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na 

Uratibu) Bi. Adela Mpina (Kulia) akifafanua jambo wakati wa 

kikao cha Wataalam kutoka Oxford Policy Management, 

Kushoto ni Mkururgenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya 

Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, 

Wanawake na Makundi Maalum tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu- Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala 

ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na 

kufanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy 

Management kuhusu Uwezekano wa matumizi ya akili bandia 

(Artificial Intelligence and Machine Learning) katika kufanya 

mapitio ya matumizi ya umma (Public Expenditure Review).


Kikao hicho kimefanyika tarehe 09 Mei 2024 ofisini kwake 

Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi amesema pia lengo la 

kikao hicho ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali 

ya mtoto (ECD) nchini Tanzania.


Ikumbukwe Serikali ya Tanzania ilizindua Programu ya Taifa 

ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali yam Mtoto (PJT-

MMMAM) mwaka 2021 kama mpango mkuu wa kuzileta 

pamoja Wizara na wadau mbalimbali ili kuboresha Makuzi na 

maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa 

miaka 8.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.