Habari za Punde

UNESCO kulifufua jengo la ‘Majestic cinema’

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ZANZIBAR Mhe.Lela Muhammed Mussa akizungumza na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Yusushi Msawa huko walipokutaka Park Khayyt  katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) ambalo litakua kituo kukuu  cha utamaduni mara baada ya kukamilika matengenezo hayo.

Na Fauzia Mussa, Maelezo.  08-05-2024

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamduni-UNESCO, zinatarajia kulifanyia ukarabati jengo la sinema Majestic lililoko ndani ya hifadhi ya  Mji Mkongwe.

Hatua hiyo inalenga kulifanya jengo hilo kuwa  kituo kikuu cha utamaduni Zanzibar.

Akifungua warsha ya kujadili mikakati ya ukarabati wa jengo hilo iliyoshirikisha timu ya wataalamu kutoka UNESCO, Japan, Saudi Arabia na hifadhi ya Mji Mkongwe katika hoteli ya Park Hayyt, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa, amesema serikali ya awamu ya nane imekuwa na mikakati ya kuhakikisha majengo yote ya kale katika Mji Mkongwe yanafanyiwa ukarabati na kurejesha haiba na taswira ya awali.

Aidha amesema kukamilika kwa ukarabati huo, kutaongeza vivutio vya utalii nchini.

Alieleza kuwa, pamoja na faida nyengine, zoezi hilo limelenga  kuliboresha jengo hilo lenye historia kubwa na kuendelea kuupa Mji Mkongwe hadhi ya urithi wa dunia.

Alisema mbali ya maonesho ya sinema, ujenzi huo utakapokamilika, litatumika kwa matukio mbalimbali ya kitamaduni, zikiwemo ngoma na filamu za asili, kurikodi kazi za wasanii na kutoa burudani nyengine za kijamii zitakazovutia watalii na wananchi.

Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania Michel Toto, alisema shirika hilo litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika mambo mbalimbali yakiwemo ya utamaduni kwa maslahi ya sasa na kizazi kijacho.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa taasisi ya ‘Hifadhi Zanzibar’ inayoshirikiana na UNESCO kufanikisha mradi huo, Tolnino Sarav alisema watahakikisha kazi ya kulifufua jengo hilo inafanyika kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Jengo la sinema Majestic lilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, na ukarabati wake unahitaji dola milioni moja hadi kukamilika kwake.

Wadau mbalimbali walioshiriki warsha hiyo, walisifu hatua ya serikali ya Zanzibar na UNESCO kuja na mradi huo, wakisema una umuhimu mkubwa kwani jengo hilo ni miongoni mwa vyanzo vya mapato.

Aidha walizishukuru serikali za Japan na Saudi Arabia, kwa kukubali kutoa fedha zinazohitajika kutekeleza kazi hiyo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa akisalimiana na Balozi mdogo wa Oman Nchini Tanzania Said Salim Al-sinawiy wakati alipofika Park Khayat kufungua warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo  lililokua la sinema(majestic ) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni Zanzibar.

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa akizungumza Jambo na Balozi WA Saudia Nchini Tanzania Yahya Bin Ahmad Okeish (wakwanza kushoto), Mwakilishi wa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto (kulia Kwa waziri Lela) na Balozi wa japan Nchini Tanzania Yusushi Msawa  wakati alipofika Park khayat kufungua warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo  lililokua la sinema(majestic ) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni Zanzibar.
Balozi wa Saudia Nchini Tanzania Yahya Bin Ahmad Okeishi akizungumza katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni baada ya matengenezo hayo,warsha hiyo ilifanyika Park khayyt Mjini Unguja
Balozi wa Japan Nchini Tanzania Yusushi Msawa    akizungumza katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni baada ya matengenezo hayo,warsha hiyo ilifanyika Park khayt Mjini Unguja
Mwakilishi wa  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto akizungumza katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni baada ya matengenezo hayo,warsha hiyo ilifanyika Park khayyt Mjini Unguja
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa akizungumza wakati  akazindua warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo  lililokua la sinema(majestic ) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni Zanzibar huko Park Khayt  Mjini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Makumbusho na mambo ya kale Maryam Mansab akichangia mjadala katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kikuu cha utamaduni baada ya kukamilika matengenezo hayo warsha hiyo ilifanyika Park Khayyti Mjini Unguja
Mkurugenzi mamlaka ya usimamizi wa mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma akichangia mjadala katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni baada ya matengenezo hayo,warsha hiyo ilifanyika Park Khayyt Mjini Unguja
Wasanii wa Ngoma ya kilua wakitoa burudani katika warsha ya kujadili mradi wa kulitengeneza upya jengo lililokua la sinema (majestic) na kuwa kituo kukuu cha utamaduni baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo,huko Park khayyt Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.