Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF),
Dk. Patrice Motsepe na ujumbe alioongozana nao.
Dk. Mwinyi ameomba
ushirikiano na CAF katika kuzikuza na kuziendeleza taasisi za michezo zikiwemo
skuli za michezo nchini kwa nia ya kufuzu vyema mashindano ya “School Academic”
kwa Zanzibar hasa ikiangaliwa kuwa Zanzibar ni mwanachama wa CAF tokea mwaka
2006.
Alisema, Serikali
imejidhatiti kukabililiana na kuondosha changamoto zinazoikumba sekta ya
michezo Zanzibar ili kufikia azma ya kufuzu mashindano ya kimataifa.
Amesema, Zanzibar inahitaji
kushiriki na kufanya vizuri kwenye mashindano ya soka makubwa zaidi duniani na
kueleza kwasasa inajivunia hatua ya sekta ya michezo ilivyofikiwa kwa kuimarika
miundombinu ya kisasa na kuahidi Serikali kufanya makubwa zaidi kwenye
kuimarisha miundombinu ya michezo nchini.
Pia Rais Dk. Mwinyi
ameushukuru uongozi wa CAF kwa kuifanya Zanzibar kuwa waandaji wa Mashindano ya
“African Academic Football Champion” kwa mwaka huu wa 2024
Kuhusu mashindano ya AFCON, yanayaorafajiwa
kuchezwa Afrika Mashariki mwaka 2027 ambayo wenyeji watakuwa Tanzania, Kenya na
Uganda, Rais Dk. Mwinyi ameondoa shaka kwa Zanzibar kuwa na kipingamizi chohote
cha kufanikisha mashindano hayo na kueleza Serikali ilivyojipanga na mashindano
hayo.
Naye, Dk. Motsepe amesifu
juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua ya kuinua sekta ya
michezo na maendeleo makubwa yaliyofikiwa Zanzibar ikiweko kuwa na Uwanja mpya
wa michezo “New Aman Coplex” wenye hadhi ya kimatafa na kukidhi viwango vyote
vya FIFA.
Pamoja na hatua nzuri
iliyopo ya ushirikiano baina ya TFF na ZFF, Motsepe pia amesifu juhudi kubwa
zinazofanywa na Rais wa ZFF, Dkt. Suleiman Jabir kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuinua Soka, Zanzibar.
Akizungumza kwenye hafla
hiyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Damas Daniel Ndumbaro
amesefu sekta ya Michezo inavyokua kwa Kasi Tanzania kutokana juhudi za
kuimarika kwa miundombinu imara ya michezo nchini.
Amesema, kuelekea AFCON 2027,
Tanzania inatarajiwa kuwa na Viwanja 11 nyenye kukidhi sifa zote za viwanja vya
kimataifa baada ya kufanyiwa maboresho na matengenezo makubwa vikiwemo Zanzibar
vitatu cha “Aman New Complex”, uwanja wa Gombani, Pemba na kiwanja kipya
kujengwa, kwa Tanzania bara viwanja nane, ukiwemo uwanja mpya wa Arusha, Dar es
Salaam, Dodoma, Mororogoro, Mbeya, Mwanza, Songea na Tanga.
Akizungumzia fainali za Kombe la Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika kwa skuli za CAF zilizoanza tangu Jumanne wiki hii ambapo
kilele chake ni leo Uwanja wa “New Aman Coplex” Zanzibar, Waziri wa Habari Vijana
Utamaduni na Michezo, wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tabia Mwita Maulid amesema, Serikali
imetimiza wajibu wake kwa kuweka mazingira yote salama kwa fainali hizo na
kuahidi kwa tayari kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa kushirikiana na
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Fainali za Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika za CAF zinafanyika chini ya udhamini mkubwa wa “Motsepe Foundation” ambayo zimewashirikisha wachezaji chini ya miaka 15 kutoka
mataifa 11 ya Afrika miongoni mwao ni Tanzania, nchi ya Afrika ya Kusini, Benin,
Genie, Kongo Brazavile, Morocco na Uganda, kwa timu za wasichana na wavulana
ambazo zilianza kwa ngazi ya taifa, zone hadi bara na Tanzania imetoa timu zote
mbili za wasichana na wavulana.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment