Habari za Punde

CCM Kigoma Wawasilisha Maoni Juu ya Vitambulisho vya Taifa kwa Waziri Masauni


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza baada ya kuwasili Ofisi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Kigoma ambapo alipata kusikiliza maoni ya uongozi wa chama mkoa ambayo yalihusu upatikanaji na usambazaji wa Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Waziri Masauni yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma ambapo alipata kusikiliza maoni ya uongozi wa chama mkoa wa Kigoma ambayo yalihusu upatikanaji na usambazaji wa Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Kutoka kulia  ni Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Wanawake wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi(CCM),Prisca Mapunda na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Abusheik Kodema.Waziri Masauni yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kigoma, Sara Kailanya akizungumza mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni aliyepo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambapo alipata kusikiliza masuala yanayohusu  upatikanaji na usambazaji wa Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA).Waziri Masauni yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.