Habari za Punde

Uzinduzi wa Taarifa za Utendaji Sekta ya Nishati Uliofanya na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia utiaji Saini mkataba wa utendaji kazi kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) jijini Dodoma. Wanaotia Saini ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (wa Nne kushoto) akiwa ameshika taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 mara baada ya kuzizindua jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na wa Nne kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.