Habari za Punde

MUDA KWA WANAWAKEKUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO


Na Jumanne Magazi 

MUDA KWA WANAWAKE
KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO.

WANAWAKE na Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimi 10 iliyotolewa na Serikali ya awamu na Sita chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassani.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar Es Salaam ,Afisa Biashara wa Manispaa ya Ubungo,Aishan Ntarukundo,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Banda la Manispaa ya Ubungo lilopo kwenye waonesho ya kimataifa ya 48 ya sabasaba.

Amesema Rais Samia ametoa fursa kwa lengo la kuwainua wanawake na vijana.

"Vijana na Wamama wasiache fursa hii,waitumie kujikwamua kiuchumi,na sisi tunawataka wakaribie ofisini kwetu waje  kujipatia mikopo"Amesema Ntarukundo.

Ntarukundo,ame ambaye pia ni Mratibu wa Maonesho,amesema Rais Samia ameonesha upendo kwa Wamama na kuwataka wanawake wasikae nyumbani wachangamkie fursa hizo .

" Mimi afisa Biashara nipo teyari  kuwahudumia ikiwemo kuwapa elimu,"Amesema Ntarukundo.

Kwa upande wake Adela Foy ambaye Mwandikishaji wa ICHF,amewaka watanzania wapende kukata bima ili ziweze kusaidia pindi wanapopata majanga .

Pia amewataka wananchi kujitokeza kwenye Banda la manispaa ya Ubungo kwenye maonesho hayo,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.