Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ajumuika na Wananchi Katika Maziko ya Marehemu Mvita Mussa Kibendera Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali  na Wananchi katika kuitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma kumuombea Marehemu Mvita Mussa Kibendera, ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali, kilichofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2024, kabla ya sala ya maiti iliyofanyika katika Masjid hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika Sala ya Maiti kumsalia marehemu Mvita Mussa Kibendera, iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, iliyofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2024.(kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Abdalla Ramadhan na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi.Alhajj Zuberi Ali Maulid na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Amani Karume.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Mvita Mussa Kibendera ,baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti,  ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali,iliyofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2024.(kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Abdalla Ramadhan na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Alhajj Zuberi Ali Maulid na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Amani Abeid Karume. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Mvita Mussa Kibendera, wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 27-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Mvita Mussa Kibendera, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa  maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 27-8-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Mvita Mussa Kibendera, alipofika nyumbani kwa marehemu Maungani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 27-8-2024 na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla, wakijumuika na Familia ya marehemu Mvita Mussa Kibendera,kuitikia dua ya kumombea, baada ya kumaliza kutoka mkono wa pole kwa familia, alipofika nyumbani kwa marehemu Maungani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 27-8-2024.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.