VIONGOZI Wateule walioteuliwa hivi karibuni
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakiwa
katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakipitia hati zao za kiapo kabla ya
kuapishwa leo 14-11-2024 (kushoto ) Mhe. Iddi Said
Khamis, ameteuliwa kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar na Ndg.
Hiji Dadi Shajak, ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar BAADHI ya Waalikwa na Wanafamilia wakihudhuria
hafla ya kuapishwa kwa Viongozi waliotwa hivi karibuni, wakati Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)
akiwaapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Iddi Said Khamis kuwa
Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika
ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Hiji Dadi Shajak,kuwa Katibu
Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi
wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza
la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS
wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi
wawili aliowateua hivi karibuni.
Viongozi
walioapishwa ni Mhe. Iddi Said Khamis, Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa baada
ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dk. Mwinyi tarehe 24, Oktoba 2024.
Kabla
ya uteuzi huo, Kadhi Iddi Khamis alikuwa Mrajis wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar.
Mwengine
ni Ndg. Hiji Dadi Shajak, Katibu Mtendaji wa Tume
ya Utangazaji Zanzibar, Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kabla
ya wadhifa huo, Ndg. Shajak alikua Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kurusha
Maudhui, Zanzibar (ZMUX). Aidha, Shajak aliteuliwa Septemba, 25 mwaka 2024
kushika majukumu mapya.
Wakizungumza
kwenye hafla ya uapisho huo, iliyofanyika Ikulu, Zanznibar, viongozi hao
walimuahidi Rais Dk. Mwinyi kuyafanyia kazi maelekezo yake yote na kuendeleza
jitihada ya taasisi mpya wanazozitumikia kwa kuendeleza ushirikiano kwa
Serikali na wadau wengine.
Hafla
ya uapisho huo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu
wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman na Mhe.
Hemed Suleiman Abdulla, viongozi wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na Masheikh kutoka
Ofisi ya Mufti, Zanzibar.
IDARA
YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment