Habari za Punde

DK.Mwinyi :Tuzitumie Rasilimali za Chama Kujijenga Kiuchumi

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi  na Viongozi wa CCM, akikata utepe kulifungua Jengo la Afisi ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini Kichama, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.  

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza  Jumuiya za  Chama hicho kuzitumia  rasilimali  vizuri kwa lengo la  kukijengea uwezo kiuchumi.

Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozindua  Jengo jipya la Afisi ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama  Cha Mapinduzi  Wilaya ya Mfenesini ,Wilaya ya Magharibi A.

Aidha Makamu Dk. Mwinyi amefahamisha kuwa Kazi za Siasa zinahitaji fedha nyingi hivyo Chama ni lazima kiwe na Miradi inayozalisha ili kujijenga Kiuchumi.

Makamu Dk.Mwinyi  ameupongeza Uongozi wa  Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya  Kichama Mfenesini kwa Kujenga Jengo la kisasa  la Jumuiya hiyo na  kuwa na  dhamira ya kuanzisha  Miradi ya Ushoni  na Ukumbi wa shughuli mbalimbali.

Halikadhalika Dk.Mwinyi ameahidi kwa Chama cha Mapinduzi kuunga Mkono  Miradi ya Kimkakati ya  Itakayoanzishwa na Jumuiya zote za Chama hicho  ili ziweze kujitegemea .

Akizungumzia suala la Udhalilishaji wa Kijinsia Dk, Mwinyi ametoa wito kwa jamii Kuanzia ngazi ya Familia kwa kila Mmoja kutimiza wajibu  wa  kukemea na kukomesha Vitendo hivyo ndani ya jamii.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.