Habari za Punde

Ufunguzi wa Nyumba ya Makaazi na Biashara Mkunazini Mnadani Baada ya Kufanyiwa Matennenezo Makubwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif (kulia)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.

Na Ali Issa.  Maelezo Zanzibar.- 09.01.2025.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwapatia wananchi wake makaazi mazuri na yalio bora bila ya kuangalia tofauti ya chama chochote cha siasa na kuweza kuendeleza Mji wa Zanzibar.

Ameyasema hayo huko Darajani Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff wakati akifunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara zilizopo Darajani Mnadani Nyumba NO 699/1705 ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema Serikali katika kuleta Makazi na maendeleo haingizi chama wala tofauti za watu bali wanaangalia kuwa wananchi wa Zanzibar wanaishi katika Makazi bora, salama na ya kisasa.

“Maendeleo yalio letwa na Mapinduzi yataendelea kuwepo kwani ujenzi wa nyumba za maendeleo na Makaazi zimeaza tangu awamu ya kwanza, kwahivyo na sisi awamu ya nane tutaendelea kujenga nyumba zilizo nzuri za Makazi na zilizo bora” alisema Sharif.

Aidha amesema Serikali kupitia Shirika la Nyumba watajenga nyumba 3000 chumbuni, wamefungua nyumba 72 kwa mchina, nane Mkungu malofa Chakechake, na Maduka 20, nyumba Tano kwa fundi Abdull na Maduka 8 Darajani, wataendelea kujenga Kikwajuni Nyumba 1095.

Nae Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar Sultani Said Suleiman amesema wamejenga nyumba hiyo kufuatia kwa uchakavu na kuhatarisha maisha ya watu ambao wengi wao walikuwa wamehama na kubakiwa na watu wachahe.

Vilevile amaaeleza ujenzi wa nyumba za Mnadani Darajani ni ukarabati wa nyumba tano na Maduka 4 ukijengwa na Kampuni ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC Company LTD) na umegharimu zaidi ya Milioni 570 ukisimamiwa na Kampuni ya ZHC consultancy.

Nae Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar Salha Muhamed Mwinjuma amesema kuwa Shirika la Nyumba kwa sasa liko vizuri na imara na litaendelea kukarabati nyumba kongwe pamoja na kujenga nyumba mpya kama agizo la Serikali lilivyoelekeza kwa Zanzibar nzima.

Mapema Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mustafa Kitwana Mustafa akitoa Salam za Mkoa amesema ujenzi wa ukarabati wa nyumba zilizopo eneo la Mji Mkongwe ni kuweka makazi salama kwa wananchi wa eneo hilo ili kuwanusuru na maafa kwa zile nyumba kongwe zilizochoka.

Aidha alimshukuru Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na Wizara ya Aridh ujezi na makazi kwa azma yao njema kuendeleza ujenzi wa makaazi bora na nafuu kwa wananchi wa Zanzibar ni jambo la kushukuriwa kwa uongozi mwema pamoja na Viongozi wasisi.

Ujenzi wa ukarabati wa Nyumba hiyo uliaza tarehe16/6/2023 na ulimaliza tarehe 30/ 12/ 2024 ambapo kuna malengo ya kujenga nyumba 548 Kisakasaka B, watajenga 240 Kisakasaka A, nyuma 209 Saateni, kwa Unguja na upande wa Pemba wanatarajia kujenga Nyumba 180 huko Mfikiwaa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif (katikati)akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa  Nyumba za Makaazi na Biashara Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif  Ali Sharif 

(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Ujenzi Shirika la Nyumba Eng,Juma 

Saleh Juma mara alipowasili katika Ufunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara 

Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya 

Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano 

kwa Maendeleo yetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif (kulia) akizungumza kitu wakati akitembelea Nyumba za Makaazi na Bishara katika Ufunguzi wa Nyumba hizo  Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.



Msanii Kirobo akitowa burudani ya igizo maalumu wakati wa ufunguzi wa Nyumba ya Shirika la Nyumba Zanzibar iliyofanyika ukarabati mkubwa kwa ajili ya Makaazi na Biashara iliyoko eneo la Mkunazini mnadani Jijini Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Sultan Suleiman akitoa Taarifa ya Kitaalamu katika hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Nyumba za Makaazi na Biashara Mnadani Darajani.Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu"Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.



Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Zanzibar wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Nyumba ya Mkurazini baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya Makaazi na Biashara, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.