Habari za Punde

Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM Wadi ya Mambosasa

Katibu wa Siasa ,Uenezina Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufungaji wa Darasa la  Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.

Na Ali Issa – MAELEZO, 3/5/2025

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, amewataka vijana waliopata mafunzo ya darasa la itikadi katika Wadi ya Fuoni Mambosasa kuyatumia vyema kwa lengo la kukijenga chama na kukipa uimara zaidi.

Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Kwenzii, Mbeto alisema kuwa kiongozi bora wa CCM ni lazima apitie mafunzo ya itikadi kwa dhamira ya kupata vijana wazalendo waliokomaa kisiasa, ili hatimaye wawe viongozi bora wa baadaye.

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwenu. Yatumieni kwa faida ya kukijenga chama, kuimarisha umoja na mshikamano. Kiongozi bora wa CCM ni yule aliyepitia na kuelewa vizuri itikadi ya chama,” alisema Mbeto.

Alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kueneza itikadi ya chama chenye sera ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano, sambamba na kuenzi misingi na maadili mema ya CCM, hatua itakayosaidia chama kuendelea kushinda majimbo yote katika chaguzi zijazo.

Awali, akisoma risala ya wahitimu wa mafunzo hayo, Katibu wa UVCCM Wadi ya Fuoni Mambosasa, Sharifa Haji Suleiman, alisema jumla ya wakereketwa 93 walishiriki mafunzo hayo – wanawake 51 na wanaume 42. Alieleza kuwa jumla ya mada tano zilifundishwa, ikiwa ni pamoja na historia ya Zanzibar, Katiba ya Chama na kanuni zake, uzalendo, athari za rushwa, na umuhimu wa kutunza siri za chama.

Sharifa alitaja baadhi ya changamoto walizokumbana nazo wakati wa mafunzo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama kompyuta, mashine ya kunakili (fotokopi), printa, pamoja na rasilimali za kuwapeleka vijana kujifunza historia kwa vitendo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Wadi ya Fuoni Mambosasa, Mohamed Ramadhani Amour, akimkaribisha mgeni rasmi, alisema kila kiongozi ana wajibu wa kuhakikisha Taifa linaendelea kusonga mbele. Alisisitiza kuwa juhudi kubwa zimefanyika kufanikisha mafunzo hayo, hivyo vijana wana wajibu wa kuwaunga mkono viongozi wao kwa namna yoyote ile kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.

Katibu wa Siasa ,Uenezina Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akimpatia Cheti cha Itikadi Saleh Hemed Matar katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Katibu wa Siasa ,Uenezina Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akimpatia Cheti cha Itikadi Farashuu Mussa Abdalla ambae ni Diwani wa Wadi ya Mambosasa  katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Katibu wa Siasa ,Uenezina Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akitoa Kadi kwa Mwanachama Mpya wa CCM Yunus Juma Rashid katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Mwenyekiti wa UVCCM Wadi wa Mambosasa Mohamed Ramadhan Amour akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni rasmi katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakionesha alama ya Dolegumba kuashiria kuunga Mkono maneno yaliotamkwa na Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Katibu wa CCM Wadi ya Mambosasa Talib Ramadhan Haji akitoa salamu za Viongozi wa CCM katika hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Katibu wa UVCCM Wadi ya Mambosasa Sharifa Hassan Haji akisoma Risala katika hafla ya  Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti Chipukizi Taifa Atka Juma Hassan akiimba Wimbo wa Mashujaa mara baada ya kuwasili Mgeni Rasmi katika Hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wakiimba Wimbo wa Mashujaa mara baada ya kuwasili Mgeni Rasmi katika Hafla ya Ufungaji wa Darasa la Itikadi kwa Wanachama wa CCM katika Wadi ya Mambosasa,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Kwezi Fuoni Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai  - Maelezo  Zanzibar.03/05/2025.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.