6/recent/ticker-posts

Vikunguni bingwa 'Mazingira Cup'

Na Haji Nassor, Pemba
TIMU ya skuli ya sekondari Vikunguni Wilaya ya Chake Chake, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Mazingira, baada ya kuishindilia skuli ya Wingwi kwa magoli 4-1, kwenye mchezo wa fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Gombani.

Magoli ya mabingwa hao, yalifungwa na Vik Yakoub, Said Malik waliozifumania nyavu katika kipindi cha kwanza, huku Abdallah Seif na Sadam Maulid wakimaliza kazi katika kipindi cha pili.

Bao la kujifariji kwa Wingwi, liliwekwa nyavuni na Haji Khamis mnamo dakika ya 70.
Kwa ushindi huo, Vikunguni ilibeba kikombe na shilingi laki tatu na skuli ya Wingwi kuramba shilingi laki mbili.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Juma Kassim Tindwa, alikabidhi zawadi kwa washindi, na kuwashajiisha kuzingatia nidhamu wanapokuwa viwanjani ili kujijengea mustakbali mzuri katika medani ya michezo, ambayo alisema ni ajira tosha kama itaendelezwa vyema.

Mashindano hayo yaliyoanza Mei 28 kwa lengo la kusherehesha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yalishirikisha timu nane kutoka skuli mbalimbali za mikoa miwili ya Pemba.

Post a Comment

0 Comments