Na Khamis Amani
BENKI ya Dunia (WB), inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa uboreshaji wa mji wa Zanzibar, ili uweze kuwa na haiba nzuri na kivutio kwa wakazi wa ndani na nje.Mradi huo ujulikanao kwa 'Zanzibar Urbarn Services Project' (ZUSP) unatarajiwa kuanza muda mfupi baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, Abeid Juma Ali, aliyasema hayo ofisini kwake Malindi alipokua na kikao na waandishi wa habari.
Alisema mradi huo utaleta mabadiliko makubwa ya haiba ya mji wa Zanzibar, ambao hivi sasa kuna kilio kikubwa cha serikali kutokana na hali yake isiyoridhisha.
Alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa mitaro ya maji machafu, michirizi, taka taka ambapo hivi sasa tayari wameshaanza kupokea vifaa mbali mbali kwa ajili ya usafi vikiwemo magari ya kusombea taka na vidampa vitakavyosaidia kurahisisha ufanyaji wa usafi.
Sambamba na huduma hiyo, mradi huo utahusisha ukarabati wa jengo la ofisi ya Baraza la Manispaa, ili liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Awali Mkurugenzi huyo alikanusha madai yaliyotolewa na wafanyabiashara wa soko la mboga mboga Mombasa, kuwa Baraza lilihusisha wanasiasa kwa ajili ya kuwaonea wafanyabiashara hao kwa kuwavunjia maeneo yao ya biashara.
Alisema kitendo cha uvunjaji wa maeneo hayo ni sahihi, kutokana na kwamba wafanyabiashara hao hawakupata ruhusa ya ujenzi kutoka Baraza ambalo ndilo lenye mamlaka ya kutoa ruhusa.
Alisema kibali walichopewa kimetoka kwa Mkuu wa soko ambaye kisheria hapaswi kutoa kibali, bali yeye alistahiki kumuarifu Mkurugenzi baadae Kamati ya Kazi, Ujenzi ya Baraza ambao wote hao walikuwa hawana taarifa.
Malalamiko ya wafanyabiashara hao waliyatoa katika kituo cha ZBC TV kwa madai wameonewa kwa kuvunjiwa maeneo yao na ilhali barua ya ombi la ujenzi waliliwasilisha kwa Mkuu wa soko hilo.
4 Comments
Ndugu Abed ali kazi kamaile ulonifanya mombasa kwenye soko la mboga inahitajika darajani kituo cha daladala, pana vurugu kubwa la wafanya biashara inakuwa usumbufu kwa abiria na waendao kwamiguu na pia usisahau umbala treni darajan, hatakipofu anaona mzingira yaliyopo barara hata pakingi zimezungukwa wafanya biashara za kutandika chini saa tisa ya mchana panuzwa samaki watu wanaachasoko wanauza bele ya maduka. Nifaraja kufikiriwa na hibenk ya dunia lakini? znz, bado hajakuwa tayari kwamipango miji kama mnafagilia uliji wa benke ya dunia sawa
ReplyDeleteSiku zote ntaendelea kusema, tatizo la Z'bar sio umaskini wa mali bali, akili.
ReplyDeleteSuala la uboreshaji mji wa Z'bar, linahitaji zaidi sheria kuliko fedha za 'World Bank'
Kwani bila ya sheria utawafanya wenye mradi badala ya kukusaidia, waanze kulipa watu fidia
Z'bar inahitaji watu mwenye uwezo wa kufikiri na kusimamia sharia zikiwemo zile za miji.
Hivi inakuwaje eneo kama la michenzani watu wanaruhusiwa kujenga nyumba za chini na za makuti?
Naaminikama sio sharia, kulazimisha maghorofa sehemu kama kariakoo(Dsm) hadi leo hii pangekua kama pale Gulioni B.o.T.
Hapo ngojea siku moja waje UNESCO na mradi wa kuondoa vibanda katikati ya mji kwa kulipa fidia, uone wahadimu watakavyo charukwa!
Utaskia kwenye maelezo baada ya khabari" ni jambo la aibu na lisilo pendeza kuendelea kuwa na nyumba zisizo na hadhi katikati ya mji wetu"
"Tunaipongeza SMZ kwa uwamuzi huu, hili ni jambo jema linalopaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu
'Inawezekana, timiza wajibu wako"
Mimi pia hujiuliza hivi lile jengo la 'treni' pale Darajani ambalo ni uso wa
mji na mna wapangaji wa maduka na makaazi ni lini lirapigwa angalau chokaa au mpaka aje mzungu?...ah kazi ipo!!!
Hayo ni matokeo ya uongozi wa kushtukizwa!
ReplyDeleteKama hujawahi kuwa na ndoto ya kuwa utaifanyia nini nchi yako au kuona mapungufu yoyote, halafu..paa, umekuwa kiongozi unadhani ungefanyaje?
Sio mnakaa kaa mnalaumu tu haya matatizo yanaanzia mbali!
Sasa viongozi wazuri waatoka wapi? ikwa nusu narobo ya wazanzibari uwezo wao wakufikri ni mdogo hujui mwenye elimu na asoelimu wote vipofu, tulifikri hawamuamsho, wata isemea jamii, hii iliyo potoka akili ilokuwa haina uwezo wakufikri, wangeiamsha, smz, na wana nchi wakajijuwa wao nani na wana wajibu gani katika kuijenga nchi yao na vizazivyao, wao kumbe ni mabedui kuliko hawa smz
ReplyDelete