Ujumbe wa wadi za Makunduchi ukiwa katika majadiliano na ujumbe wa Manispaliti ya Kiruna kabla ya kuanza ziara yao ya kutembelea vianzio vya maji pamoja na mitambo ya kusafisha maji. Ujumbe unauwakilishi wa chama cha CCM na CUF. Upande wa kushoto wa tatu ni ndugu Simai Ameir Haji kutoka CUF ambaye pia ni mtaalamu wa maji na pia ana shahada ya sayansi katika kompyuta. Mjumbe anayefuatia ni bwana Moh'd Simba anayewakilisha CCM. Watu wa Makunduchi wameamua kushughulikia maendeleo na kuacha nyuma siasa za visiwani .
Semina ya maji ambayo ujumbe wa watu wa Makunduchi walihudhuria nchini Kiruna SwedenKatika picha kutoka kushoto ni Ndugu Mohamed Muombwa, Simai Ameir Haji, Mwalimu Haji Kiongo, Moh'd Simba, Hafsa Makame na afisa tawala wa wilaya Kusini, ndugu Abdalla Ali Kombo. Ujumbe huo unapata maelezo kuhusu namna ya kusafisha maji katika manispaliti ya Kiruna.
Ndugu Moh'd Simba pamoja na afisa tawala Abdalla Ali Kombo wakiangalia jinsi ya mitambo ya kusafisha maji Kiruna Sweden
Kutoka kulia ni bi Mwatima Hassan ambaye atakuwepo Kiruna kwa kipindi cha mienzi 4 kutoa mafunzo ya kiswahili na utamaduni kwa walimu watakaokuja Makunduchi kusomesha wanawake 12 katika ujasiriamali, kompyuta, kiingereza. Mafunzo hayo ya mwaka mmoja yataanza Januari 2014.
1 Comments
Sasa hawa Jamaa kutoka Makunduchi watawaletea nini wananci wao!!? wache wakataalii warudi zao.
ReplyDelete