6/recent/ticker-posts

China Yaikabidhi Msaada wa Matrekta aina ya Power Tiller 8 ZAYEDESA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman,akihutubia wakati wa sherehe za makabidhiano ya Matrekta ya Kilimokwa Junuiya ya Vijana Inayojishughulikia Maendeleo ya Vijana Elimu na Mazingira Zanzibar (ZAYEDESA) msaada uliotolewa na Serekali ya China kwa jumuiya hiyo, makabidhiano hayo yamefanyika huko Tunguu.  
 Balozi Mdogo wa China Balozi Xie Liu Yaung, akihutubia katika sherehe hiyo kabla ya kukabidhi matrekta hayo kwa jumuiya hiyo huko Tunguu katika shamba la Elimu ya Kilimo kwa Vijana.
 Mjumbe wa Bodi ya ZAYEDESA, Maryam Hamdan, akitowa shukrani kwa Balozi wa China Zanzibar kutokana na msaada huo waliokabidhiwa na Balozi huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt. Idris Muslim Hija. akitowa shukrani kwa China na Jumuiya ya ZAYEDESA kukabidhiwa Matrekta hayo na wao kuyagawa kwa Wizara ya Kilimo na Jeshi la Mafunzo ili kuendeleza kilimo cha Mpunga Zanzibar, Wizara ya Kilimo imepewa matrekta 4 na Mafunzo mawili na mawili kubaki kwa Jumuiya hiyo ya ZAYEDESA kwa kilimo cha mpungu.
 Maofisa wa Mafunzo na Wizara ya Kilimo wakimsikiliza Balozi wa China alipokuwa akihutubia katika sherehe hiyo ya makabidhiano ya Matrekta ya aina ya Power Tiller.

Balozi wa China Xie Yun Liang, akimkabidhi Matrekta Waziri Haroun Suleiman,kwa ajili ya Jumuiya ya ZAYEDESA, na jumuiya hiyo kuyagawa kwa Wizara ya Kilimo na Jeshi la Mafunzo Zanzibar.
Waziri Haron akimkabidhi Afisa wa Chuo cha KilimoKizimbani matrekta 4 kwa ajili ya Kilimocha Mpunga, akishughudia ni Balozi wa China Xie Yun Liang

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman, akimkabidhi  Matreka 2 kwa ajili ya kulimo kwa Jeshi la Mafunzo Zanzibar, Kamishna Msaidizi Muandamizi Ali Abdalla Ali, katikati Balozi Mdogo wa China Xie Yun Liang, matrekta hayo ymetolewa na Serekali ya China kwa Jumuiya ya ZAYEDESA na jumuiya hiyo kuyagawa kwa Jeshi la Mafunzo na Wizara ya KilimoZanzibar, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vha shamba la ZAYEDESA Tunguu

Baadhi ya Power Tiller waliokabidhiwa Jumuiya ya ZAYEDESA na wao kuyagawa kwa Wizara ya Kilomo na Jeshi la Mafunzo, kwa ajili ya Kilimo cha Mpunga katika mabonde mbalimbali yalioko Unguja na Pemba.

Post a Comment

1 Comments

  1. Hayo yote yataishia Kwa Akina CCM na Wahafidhuna kama yale Metrektor waliokabidhiwa Masheha Uchwara..Yalikua yanawalimia watu wa CCM.

    ReplyDelete