Muwezeshaji kutoka Unicef Tanzania Mtaalamu wa masuala ya HIV AIDS, Godfrey Yikii, akitowa mafunzo kwa Wafanyakazi wa jumuiya ya ZAYEDESA, kuhusiana na kutowa ushauri Nasaha kwa Vijana wa makundi hatarishi kuhusiana na TB, Ukimwi, na Dawa za Kulevya, mafunzo hayo yameandaliwa na Unicef kwa kushirikiana na Jumuiya ya ZAYEDESA, yaliofanyika katika ukumbi wa kituo cha ushauri Nasaha Miembeni.
Muwezeshajin kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja, akitowa mada kuhusiana na maambukizi katika mafunzo ya siku tano ya kutoa Nasaha kwa Vijana walioko katika makundi hatarishi kutokana na Maradhi ya TB, Ukimwi na Dawa za Kulevya.
Mratibu wa Mafunzo wa Jumuiya ya ZAYEDESA Mgoli Lucian, akitowa maelezo kuhusu mafunzo hayo kwa Wafanyakazi wa ZAYADESA, jinsi ya kuyatumia mafunzo hayo waliopewa na jinsi ya kufanya kazi wakiwa katika vituo vya Kazi,jumla ya Wafayakazi wa jumuiya hiyo wa Vituo vya Pemba, Nungwi, Paje na Miembeni walipata mafunzo hayo yalioandaliwa na Unicef kwa kushirikiana na ZAYEDESA.
Wafanyakazi wa Vituo vya Ushauri Nasaha vya ZAYADESA wakifuatilia mafunzo hayo yalioandaliwa kwa ajili yaokupata elimu ya kufanikisha kazi zao kwa kutowa huduma ya Ushauru Nasaha, wanapofika katika vituo hivyo kupata huduma ya Ushauri Nasaha.
0 Comments