Huu ndio Mnara unaotarajiwa kujengwa katika Viwanja vya Michenzani kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi unatarajiwa kuanza ujenzi wake kuanzia sasa na kuwa Kivutio cha Watalii wanaokuja kutembelea Zanzibar kama ilivyo sehemu nyengine za Dunia kuwekwa sehemu ya kumbukumbu ya matukio muhimu.
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ inakusudia kujenga mnara
maalum utakaotoa kielelezo cha
kumbukumbu ya miaka 50 tangu yafanyike Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.
Januari 12 mwakani Zanzibar
itaadhimisha kutimia miaka 50 tangu kufanyika kwa mapinduzi ya mwaka 1964
ambayo yaliuondosha utawala wa Sultani .
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Vuga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, ujenzi
wa mnara huo utaambatana na ujenzi wa kituo cha ukuzaji uchumi ambacho kitakuwa
na uwezo wa kutoa ajira ya watu 80.
Waziri Aboud alisema mnara huo unatarajiwa kujengwa katika
eneo la Muembekisonge karibu na na jingo la maendeleo la michezani jumba namba
2, ambapo hivi sasa limekuwa limekuwa likitumiwa kwa ajili ya mapumziko.
Alisema mnara huo unajengwa katika eneo hilo kwani ni kitivo na chemchem ya
maandalizi yaliyofanikisha kufanywa kwa mapinduzi hayo.
Waziri huyo, amesema ujenzi huo wa kumbukumbu hiyo, utaenda
sambamba na kuligeuza eneo hilo kuwa la kiuchumi, kutokana na mnara huo
utaambatana na ujenzi wa maduka ya kisasa pamoja na shughuli za kukuza utalii
Zanzibar na kumbukumbu ya Mpapinduzi ya
Zanzibar.
Alisema Serekali ya Mpinduzi Zanzibar inatarajia kutumia
zaidi ya shilingi bilioni moja, ambazo zitatokana na viazio mbalimbali ukiwemo
mchango wa Serekali na Taasisi binafsi na kusimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar ZSSF.
Alisema ndani ya ujenzi wa mnara huo, unatarajiwa kuwa na
maeneo ya kuweka kumbukumbu ya shughuli za Mapinduzi zikiwemo zana zilizotumika
wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar jambo ambalo
litavutia watalii wanaotembelea Zanzibar.
Aidha alisema eneo jengine ndani ya mnara huo, linakusudiwa
kuwekwa mikahawa na ukumbi mkubwa wa kufanyia shughuli mbalimbali,jambo ambalo
linaweza kusaidia kukuza Utalii wa Zanzibar.
Akiendelea Waziri Aboud alisema ujenzi huoutaenda sambamba
na kulifanyia mabadiliko eneo hilo
kwa kuruhusu kuwepo kwa bustani mpya ya mapumziko pamoja na eneo la uegeshaji
wa magari.
Mhe. Aboud alisema mabadiliko hayo yatahusisha ujenzi wa
jingo jipya la kituo kikuu cha biashara kwa kejenga maduka makubwa (super market),ambayo itaweza kupunguza na kutoa
ajira kwa watu zaidi ya 80, ikiwa ni hatua itakayosaidia kupunguza mrudikano
katika eneo la darajani.
Alisema Serekali imeamua kuweka mnara huo, ikiwa ni sawa na
mfumo wa baadhi ya mataifa duniani, ambayo yamekuwa na vielelezo vya aina hiyo,
ikiwemo Paris, Ufaransa na Shangai China.
Kutokana na kuwepo kwa dhamira hiyo, Waziri Aboud aliwatakaka
wananchi kuiunga mkono serekali katika ufanikishaji wa ujenzi wa Mnara huo,
pale kazi zitakapoaza kwa kutofanya bughu mahali hapo.
Alisema serekali inachokifanya ni kuona eneo hilo linaimarishwa zaidi kuwa la kisasa na lenye
kuiwezesha Zanzibar
kukuza Uchumi na Utalii wa nchi kwa vile inatarajiwa kuwa ni kivutio kikubwa
kwa mataifa mbalimbali duniani.kujua historia ya nchi hii.
Waziri Aboud alieleza wanatarajia kuona kazi hiyo
inakamilika katikamwezi wa Januari, lakini inawezekana kuwa endelevu baada
yakipindi hicho kupita kutokana na
ramani ya shughuli hizo kuhusisha mambo mengi na itakachoaza nacho ni kuweka
jiwe la msingi.
Kutokana na mipango hiyo ya Serekali Waziri Aboud, pia
aliwaombawananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za sherehe hizo zikiwemo
za kujitayarisha kushiriki katika
maonesho ya aina yake yatakayofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa
SUZA kampasi ya Beit –el raas.
Amesema katika maonesho hayo serekali inatarajia kuonesha
shughuli mbalimbali za Taasisi za Serekali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuonesha
mafanikio yaliopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

1 Comments
Zssf kujenga vitu kama hivi sio vibaya, ikiwa mtafanya akili kutumia pesa zetu kwa njia ya uadilifu, kuna miradi mingi sana katika nchi hii inatakiwa tuifikirie, mfano kuwekeza hizi pesa zetu kwenye kujenga nyumba za makaazi na kukodisha kwa bei nafuu. tunahitaji muchangie kwenye miundo mbinu ambayo watu watakuwa wanaitumia kwa kila siku, kujenga garden na mambo mengine ila kukaa na pesa bila ya kuona mradi wowote haisaidii kitu wakati tunajua wazi kuwa pesa zipo nyingi tu.
ReplyDelete