6/recent/ticker-posts

Sheikh Azan aanza matibabu nchini India

Hatimaye Kiongozi Mwandamizi wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya kiislamu Zanzibar(JUMIKI) Sheikh Azan Khalid Hamdan ameanza kupatiwa matibabu nchini India ambapo jumla ya vijiwe 17 vimeonekana katika mafigo yake na madaktari wamefanikiwa kuviyeyusha vijiwe vya upande wa kushoto.

Kwa mujibu wa taarifa fupi aliyoituma Sheikh Azan, amesema baada ya muda wa wiki moja ataendelea na matibabu ya mafigo ya upande wa kulia.

Aidha, Sheikh Azan amewashukuru watu wote wanaoendelea kumtumia ujumbe mfupi wa kumtakia pole, na kuahidi kuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, matatizo yake yatapatiwa ufumbuzi nchini humo.

Hata hivyo amesema bado hajafanya vipimo vya tumbo na kichwa, bali amepatiwa baadhi ya masharti ikiwemo kutofunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa muda wa miaka mitatu mfululizo pamoja na kupunguza matumizi ya kupiga na kupokea simu.

Sheikh Azan amesema maelekezo mengine kapatiwa Daktari wake aliyeambatana naye nchini humo, kwa vile baada ya kutoka katika mashine alipoteza fahamu kutokana na maumivu makali na kupigwa sindano.

"Masharti niliyopewa nisifunge Ramadhan miaka mitatu na nipunguze upigaji wa simu, mengine kaambiwa daktari wangu, mimi baada ya kutoka kwenye mashine nilipoteza fahamu kwa maumivu makali na kupigwa sindano" alisema Sheikh Azan katika taarifa yake aliyoituma kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi.
 
Taarifa kutoka kwa Munir Zakaria

Post a Comment

1 Comments

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete