6/recent/ticker-posts

Hali Halisi ya Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi Jangwani Jijini Dar Jana.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakimsubiri Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya Urais. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam alipowasili katika viwanja vya jangwani kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania.
Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya jangwani.
           Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na DC wa Kinondoni.
         Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano jangwani.

Wasanii wakitowa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Urais wa Chama cha Mapinduzi Dk John Magufuli jangwani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Mnauye akitowa utaratibu wa Uzinduzi wa Kampeni za Urais katika viwanja vya jangwani Dar. 
Wake wa Viongozi wa Serikali wakiwa katika hafla ya mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni viwanja vya jangwani jana Mwenye miwani Mke wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Asha Bilal Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Anna Mkapa na Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Siti Mwinyi. wakihudhuria mkutano huo.

Wasanii wa Bandi ya Yamoto wakifanya vitu vyao jukwaani katika viwanja vya mkutano jangwani Dar. 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Viwanja vya jangwani Dar.

            Kiongozi wa Wafanya Biashara ndogondogo akizungumza katika mkutano huo jana
Kiongozi wa Umoja wa Bodaboda Dar-es-Salaam akizungumza wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika viwanja vya Jangwani Dar jana. 

Mwananchi akipata kumbukumbu ya picha ya umati wa Watu katika viwanja vya jangwani kupitia simu yake ya mkononi ili kupata kumbukumbu hiyo haijawahi kutokea katika medali ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi.
Makongoro Nyerere akitembea kwa bwaride baada ya kuzungumza na wananchi wa CCM wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM Jangwani jana, 
Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Jaji Joseph Warioba akihutubia wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofantika katika viwanja vya jangwani Dar.
Waziri Mkuu Mstaaf Jaji Joseph Warioba akipongezwa na Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli baada ya kumaliza kuhutubia yake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa Urais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli katika viwanja vya jangwani Dar jana.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya jangwani wakihudhuria mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika katika viwanja hivyo.
Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Al hajj Ali Hassan Mwinyi (Mzee Ruhusa) akiwahutubia WanaCCM katika viwanja vya jangwani Dar wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya jangwani jana Dar. 

Rais Mstaaf wa Tanzania Benjamin Mkapa akiwahutubia WanaCCM katika viwanja vya jangwani katika mkutano wa kampeni za CCM kwa mgombea wa Urais. 


Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombe Urais wa Tanzania kupitia CCM John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam jana(kushoto)Mgombea mweza Samia Suluhu Hassan ,






Post a Comment

0 Comments