SERIKALI ya Zanzibar, imesema itafanya mazungumzo na Jeshi la Polisi ili waanzishe utaratibu wa kutumia usafiri wa mabasi kwa ajili ya mahabusu wanaofikishwa Mahakamani badala ya magari makubwa maarufu makarandinga.
Hatua hiyo ya serikali imekuja kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha huduma za vyuo vya mafunzo, ikiwa pamoja na kuzungumza na Jeshi hilo ili kubadili magari hayo.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame, aliyasema hayo barazani jana wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Wanawake, Shadya Mohammed Suleiman aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kuimarisha huduma za usafiri wa kisasa kwa ajili ya mahubusu .
Waziri Mwinyihaji alisema ni kweli kumekuwa na mabadiliko ya usafirishaji mahabusu kwa upande wa Tanzania bara, kwa kutumia usafiri wa mabasi madogo lakini mpango umekuwa ukitekelezwa kwa majaribio kwa Mji wa Dar es Salaam.
Alisema utaratibu wa kupeleka mahabusu Mahakamani upo chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi serikali ya Zanzibar italiangalia ili liweze kutekelezwa hapa.
Waziri huyo alisema tangu kuanza kutumia njia hiyo bado uko kwenye majaribio na zoezi hilo likifaa, Jeshi la Polisi Tanzania litaendeleza mpango huo katika mikoa mingine ikiwemo Zanzibar.
Waziri huyo alisema serikali ya Zanzibar katika bajeti ijayo ya fedha inajiandaa kuweka mkakati wa kuimarisha utoaji wa huduma bora ndani ya Vyuo vya Mafunzo likiwemo suala la usafiri.
"Jeshi la Polisi Tanzania litaendelea mpango huo katika mikoa mingine ikiwemo Zanzibar" !!!!
ReplyDeleteJamani kusema hivyi inamaanisha kuwa Zanzibar ni mkoa kama mikoa mengine ya Tanzania au vipi?!!
Wallahi mie huwa nachukia nikisikia nchi yangu kubadilishwa na kuitwa mkoa.
Huo uchungu wako uhamishie kwenye mambo mengine ya maana.ZNZ kuitwa mkoa ni jambo dogo sana! na haibadlishi chochote ktk hadhi ya visiwa hivi!
ReplyDelete