Habari za Punde

UJUMBE KUTOKA CHINA WAWASILI ZANZIBAR

Na Maelezo Zanzibar 21/10/2011

Ujumbe wa watu 12 kutoka Wizara ya Afya ya Mkoa wa Jiang su China ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jimbo hilo Zhou Zhengxig umewasili Zanzibar leo asubuhi kutoka China.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ujumbe huo umepokewa na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Chen Qiman,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi, na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara hiyo Juma Rajab pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa China Zanzibar.


Ujumbe huo unatarajiwa kutia Saini Waraka wa Makubaliano na Wizara ya Afya ambapo wanatarajiwa kuleta vifaa vya upasuaji mdogo na Sehemu ya upasuaji wa Mdomo maarufu kama Kisungura.

Kesho ujumbe huo unatarajiwa kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein.

China imekuwa na mahusiano mazuri na Zanzibar kwa muda mrefu ambapo nchi hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ikiwemo Afya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.