Habari za Punde

DK SHEIN APONGEZA MIAKA 40 UAE

Na Rajab Mkasaba, Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Falme za Kiarabu (UAE),Sheikh Khalifa bin Zayd Alnahyan na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtum kwa kusherehekea miaka 40 ya Umoja wa nchi hiyo.

Dk. Shein pia, amewatumia salamu kama hizo Watawala wengine wa Falme za Kiarabu.


Katika salamu hizo ambazo Dk. Shein amezituma kwa niaba yake, Serikali na wananchi wa Zanzibar na kuahidi kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na nchi hiyo utaimarishwa zaidi.

Salamu hizo zilitoa heshima kwa viongozi waasisi wa Umoja huo akiwemo marehemu Sheikh Zayid Al Nahyan na Marehemu Rashid Al Makhtum pamoja na kumwombea rehma kwa Mwenyezi Mungu viongozi hao.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitilia mkazo kudumisha mahusiano hayo hasa katika sekta za maendeleo zikiwemo biashara, uwekezaji na uchumi kwa jumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.