KAMPUNI binafsi zimelalamikia baadhi ya watendaji wa taasisi za usafiri wa vyombo vya baharini kwa kutokuwa makini katika utendaji wao kwani hupelekea kuiyumbisha serikali.
Alisema serikali imekuwa ikiyumba katika kutoa taarifa kuhusiana na vyombo vya baharini hali inayoisababishia jamii kutoelewa taarifa sahihi ya utumiaji wa vyombo hivyo.
Hayo yameelezwa na meneja uendeshaji wa kampuni ya JAK enterprise, Ali Yussif Abdalla alipozungumza na mwandishi wa habari hizi hapo Malindi.
Alisema kuzuiliwa vyombo kiholela visifanye kazi bila ya makosa ambayo yanawezesha kuhatarisha usafiri wa vyombo hivyo husababisha matatizo kwa watumiaji na kutoa taarifa si sahihi wanapokuwepo ndani ya boti hizo.
''Juzi tu boti ya Mv Kalama imerejeshwa bandarini tena na haina tatizo lolote kama viongozi waliopo Mamlaka wanaijuwa kazi yao hali ile isingetokea”, alisema Meneja huyo.
Alisema kuwa mapungufu yanayojitokeza kwenye meli hayamruhusu kuizuia meli ila kutakiwa asawazishe marekebisho yaliojitokeza.
Pamoja na hayo aliishauri serikali kutafuta ajira mbadala kwa wananchi wa Pemba ili kupunguza wingi wa abiria wengi waendao na kurudi Pemba kila siku.
Alifahamisha kuwa sababu ya kutokuwepo soko lenye kuridhisha kuuza bidhaa zao kisiwani huko husababisha wananchi hao kutotulia sehemu moja.
Pia alisema tatizo sio vyombo vya usafiri bali ni abiria wa Pemba hawana utaratibu mzuri wa kusafiri jambo ambalo linapelekea kuwa na vurugu kubwa katika chombo.
''Tatizo la Pemba ni abiria wenyewe mtu hawezi kusafiri peke yake mtu mmoja ana watoto tisa na wote hawakatii tiketi serikali hili wanalitizamaje”, alisema.
Ndugu Ali Yussuf Abdalla. Kwanza, majibu yako yana jazba sana na wewe umelalia mno kwenye maslahi yako na si usalama wa abiria. Pili, suala la Serikali kutafuta ajira ya watu wa Pemba wala kutokuwepo soko la kuuza bidhaa ni nje ya mada, na wala haihusiani na suala la usalama wa abiria. Tafadhalini fuateni sheria
ReplyDelete