Na Madina Issa
SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), limewataka viongozi wa ngazi mbali mbali nchini wajitahidi kufuata sheria za kazi pamoja na kutandika miongozi itakayoondosha migogoro katika sehemu za kazi.
Katibu Mkuu wa ZATUC, Khamis Mwinyi Mohammed alieleza hayo jana ofisini kwake Kikwajuni mjini hapo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akielezea changamoto katika sehemu za kazi.
Alisema matatizo na migogoro katika sehemu za kazi itaondoka endapo viongozi watazifuata na kuzisimamia sheria kazi sambamba na kutandikwa kwa miongozo mizuri itayoondosha matatizo hayo.
Alifahamisha kuwa hivi sasa wapo baadhi ya viongozi wamekuwa na mtazamo hasi dhidi vyama vya wafanyakazi jambo ambalo haliwezi kuleta maendeleo na ufanisi kwenye maeneo ya kazi.
“Viongozi wahakikishe wanasimamia sheria za kazi na sio kuonyesha chuki za wazi kwa vyama vya wafanyakazi jambo ambalo haliwezi kuleta tija”,alisema katibu.
Katibu huyo alisema ni wakati kwa viongozi wa kisiasa kuhakikisha wanatimiza ahadi zao walizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ikiwemo ushirikishwaji wa vyama vya wafanyakazi pamoja na kuinua
maslahi ya watumishi.
Mwinyi alisema katika mwaka huu mpya, bado kunachangamoto mbali mbali zinazowakabili wafanyakazi na taasisi za kazi akitoa mfano wa vitendea kazi kwa watumishi.
Alifahamisha kuwa ili watumishi waweze kuleta tija katika maeneo yao ya kazi, ni lazima waajiri wakawapatia vifaa vya kisasa.
Akizungumzia kwa upande wa watumishi kwa mwaka mpya, katibu huyo aliwataka wajitume kwa bidii, juhudi na maarifa ili waweze kuleta tija.
Alisema endapo watendaji watajituma kama inayotakiwa, kwa kiasi kikubwa madai ya ongezeko la maslahi kwa waajiri.
No comments:
Post a Comment