Habari za Punde

Serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la maji

Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM

SERIKALI imeweka kipaumbele kutataua tatizo la maji nchini ili kupunguza vifo kwa watoto hasa maeneo ya vijijini.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Maji, Injinia Gerson Lwenge kwenye kufunga mkutano wa nne uliojadili Sera ya maji Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

Injinia Lwenge alisema kutokana na tatizo la maji limechangia kuathiri watoto hasa maeneo ya vijijini kupoteza maisha kwa kuwa wanapata magonjwa ya miripuko kama kuhara.

Hatahivyo alidai kuwa katika maeneo ya vijijini walibaini kuna ukosefu wa vyoo hivyo unachangia watoto wengi kupata huduma katika maeneo hatarishi bila kutumia maji.

Alisema anashukuru (UNESCO) kushirikiana na wataalam wa maji kutoka nchi mbalimbali ili kuangalia namna ya mbambali za kutatua changamoto zinazokabili sekta hiyo.

Naye Katibu Mtendaji wa Kamishena ya Kamati ya Kitaifa ya Mpango wa Maji chini ya (UNESCO) Prof.Elizabeth Kiondo alisema kuwa katika mkutano huo wameazimia kufanya tafiti za ukaguzi wa kuangalia maeneo gani yanafaa na yanaweza kupatikana maji.

“Tatizo la maji limekuwa likiathiri sana kina mama hasa meneo ya vijijini kwa kuwa wanatafuta maji katika umbali mrefu”,alisema Prof. Kiondo

Prof .Kiondo alisema katika mkutano huo walibaini kuna upungufu wa wataalam kinamama katika sekta ya maji hivyo hakunabudi kuwahamasisha kujihusisha katika suala la maji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.