Joseph Ngilisho,Arusha
WATALII wawili raia wa Ujerumani, Sibflle
Ytzerott na Hans Joachim
Zenk, wamenusurika kuuawa kwa kupigwa risasi na
mlinzi wa hifadhi ya wanyama ya
Tarangile, baada ya risasi kupiga kwenye gari
namba T. 838
BAE aina ya Land Cruser, walilokuwa wamepanda na
kuliharibu vibaya.
Akisimulia kwa masikitiko, dereva aliyekuwa
akiendesha gari hilo,
lililokuwa limewabeba watalii hao, Emmanuel Chao
alisema
aliondoka
mjini Arusha na kwenda katika hifadhi hiyo Julai mosi mwaka
huu, saa 10.30 na kukata kibali cha kuingia
hifadhini, ambayo kwa
kawaida inaiisha ndani ya masaa 20 tangu kukata.
Chao alisema kuwa wakati akienda katika kibanda
hicho kukata kibali mlinzi alianza kumfokea huku akiikoki silaha yake na
kumwamuru dereva wa gari hilo
alale chini na huku akimwelekezea silaha yake
kichwani kwake, wakati
huo wazungu wakilia na kupiga kelele kwa tukio
hilo.
Chao alisema baada ya tukio hilo walitokea
madereva wenzake na kumwokoa,hata hivyo wakati akiondoka mlinzi hiyo
alilimiminia risasi gari lake lililokuwa limepakia wageni hao ,ambapo baadae
alienda kwenye kituo cha kidogo
cha polisi cha Minjingu, kutoa taarifa za
kutishiwa kuuwawa na
kuharibiwa gari lake.
Nao wageni hao, wakisimulia tukio hilo kwa lugha
ya kijerumani huku akitafsiri
Esau Malisa, walisema wamesikitishwa na kitendo
cha mlinzi wa
hifadhi kupiga risasi gari lao na kusababisha
uharibifu na
kumtishia kumuua dereva wao.
Walisema wao wanakuja nchini kuleta fedha, ila
wanashangaa wanaanza
kutishiwa maisha yao hali inayowatia wasiwasi
mkubwa na kutaka hifadhi
hiyo kumchukulia hatua stahiki mlinzi huyo kabla
ya wao kuondoka
kurudi Ujerumani.
Watalii hao walisema wametembelea hifadhi ya
Serengeti, Manyara,
Ngorongoro na Tarangile, ila kote kulikuwa na
usalama wa kutosha
Isipokuwa katika hifadhi ya Tarangile.
Naye Mwongoza watalii, Esau Malisa, alisema kuwa
mlizni huyo alitumia
silaha kali na nzito kama ya kivita, licha ya
gari hilo kuwa
lilisimama na taa zilikuwa zinawaka kuashiria
kuna gari.
Kwa upande wa
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi Tanzania, (TANAPA) , Paschal
Shelutete, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulichukua hatua stahiki
kwa
muhusika.
Pia alisema kuwa tayari wamewaandikia barua watalii
hao kuomba radhi
kwa yaliyowapata na kujaribu kuwaelewesha ili
wasisite kuja Tanzania
wakati mwingine.
No comments:
Post a Comment