Kifaa chengine kimeingia jamvini kuvinjari katika kutoa habari za Zanzibar
Kitembelee ukipata nafasi
Na Geofrey Kimbitikiri
Wazanzibari waishio nje na ambao jamaa zao
walipoteza maisha yao na wengine kuathirika katika msiba wa kuzama boti ya MV
Skagit, wamesikitika kwa kitendo cha aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambae pia ni mwakilishi wa jimbo la Ole,
wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, Bw. Hamad Massoud Hamad, kwa kuwaomba radhi
wapiga kura wake, wa jimbo la Ole kwa uamuzi wake wa kujiuzulu bila ya kuwaomba
radhi wale jamaa waliopoteza ndugu zao katika msiba wa meli hio.
Kutokana na taarifa waliyoitoa kupitia Blog
la Wazanzibari waishio nje liitwalo ZANZIBAR NI KWETU, Wazanzibari hao wamesikitika sana na kueleza kuwa wa kuombwa radhi
walikuwa ndugu na jamaa ambao walipoteza maisha yao au kuathirika kwa kuzama
meli hio ya MV Skagit.
" Kuomba radhi kwa kujiuzulu uwaziri
baada ya makosa kutokea sio ukomavu bali ni siasa ya kikaragosi. Ingelikuwa
vizuri kama Bw. Hamad angelifahamu kuwa wananchi hawamchagui Mwakilishi ili awe
waziri.
Kama Bw. Hamad angelijiuzulu uwakilishi hapo alikuwa mwenye sababu
nzito ya kuwaomba radhi wapiga kura wake wa Ole, lakini sio kwa kujiuzulu
uwaziri baada ya makosa kutokea chini ya uongozi wake. " walimalizia
Wazanzibari hao kwenye taarifa yao fupi.
Source: www.zanzibarnikwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment