Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Masheikh waliofika nyumbani kwakeMbweni kwa ajili ya kufutari nae. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad jana alijumuika pamoja na masheikh mbali mbali wa Zanzibar katika futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao wadini.
Akizungumza katikahafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni, Maalim Seif aliwataka masheikh hao kuendeleza utamaduni wa kufutarishana na kuurithisha kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Amesema utamaduni huoni wa kihistoria kwa Zanzibar na umekuwa na manufaa makubwa katika kujengaumoja, mshikamano na maelewano miongoni mwa waislamu.
No comments:
Post a Comment