Habari za Punde

Bodi ya tume ya utangazaji yazinduliwa

 Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar Chande akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kuizindua Bodi ya nne ya Tume ya Utangazaji katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Tume hiyo Kikwajuni mjini Zanzibar.
 Waziri wa Habari Utamaduni utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akitoa nasaha zake kabla ya kuizindua Bodi ya nne ya Tume ya Utangazaji Zanzibar katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Tume hiyo Kikwajuni mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Bodi ya nne ya Tume ya Utangaaji ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akipokea nyenzo za kufanyia kazi kwa Bodi hiyo kutoka kwa Waziri wa Habari Utamaduni utalii na Michezo Said Ali Mbarouk
Mwenyekiti wa Bodi ya nne ya Tume ya Utangaaji ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akitoa shukrani kwa kuteuliwa na kuahidi kufanya kazi ipasavyo katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo Kikwajuni mjini Zanzibar.

Na Mwanaisha Muhammed Maelezo Zanzibar 20/12/2012.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema kuwepo kwa magazeti mengi katika nchi kunasaidia sana kuharakisha harakati za Maendeleo .
Aliyasema hayo huko ofisini kwake Kikwajuni wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na wajumbe wa Bodi ya ushauri wa Magazeti na Vijarida Zanzibar .
Waziri alisema kwa sasa Zanzibar magazeti yaliyopo ni machache mno kilinganisha na nchi nyengine kama Tanzania Bara, hivyo kutokuwepo kwa Magazeti mengi kunadumaza maendeleo

Aliitaka bodi hiyo kutokuwa wakali wakati wa kusajili magazeti hayo na daima wawe wanawafahamisha wenye magazeti pale wanapokosea na wasichoke ila tu wakiona muhusika hafahamishiki ndipo hatua za kisheria zichukuliwe.
Amesema kuwa jukumu kubwa kwa hivi sasa kwa bodo hiyo kihakikisha inasajili magazeti ya kutosha pamoja na vijarida kwa mujibu wa sheria na taratibu ziliopo ili Zanzibar iweze kupiga hatua za maendeleo kwa kuwa na magazeti mengi kama ilivyokuwa siku za nyuma..
Hata hivyo Waziri alisema bodi inakazi muhimu katika nchi kwa kuhakikisha kwamba magazeti yatakayo ruhusiwa yawe ni yenye uhakika na sio ya kubahatisha na kuleta mfarakano katika jamii.
Nae kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambae pia ni Mshauri wa Rais wa masuala ya Utalii Issa Ahmed Othman alisema kuwa madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo ni uangalizi wa magazeti na vijarida ili yasikiuke taratibu na sheria zilizowekwa .
Alisema kuwa kwa upande wa Bodi hiyo huwa hawapitishi gazeti wala majarida kama vigezo husika vya kisheria havijakidhi haja kama sheria ilivyoelekeza ili kuepusha migogoro kutotokea katika jami
Mwenyekiti huyo alisema kuwa bodi inaona choyo kwa wazanzibari kutokuwa na magazeti mengi hivyo inakaribisha kwa watanzania kwa ujumla kuanzisha magazeti ili maendeleo yaweze kupatikana Zanzibar.
Alisema kuwa Serikali imeweka chombo cha kushughulikia vyombo vya Habari sio kuwabana bali ni kuweka utaratibu ambao utasaidia utendaji mzuri wa kazi za waandishi wa habari .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.