Na Mwandishi wetu, Dodoma
SPIKA wa Bunge, Anna Makinda
ataunda Tume maalum itakayokwenda Mkoani Mtwara kusikiliza maoni ya
wananchi kuhusu mgogoro wa gesi unaoendelea.
Akiahirisha kikao cha jana cha Bunge, Spika Makinda alisema tume hiyo
itasikiliza wadau wote katika mgogoro huo ambao ni wananchi wa Mtwara ambao
wanapinga gesi hiyo kutosafirishwa kwenda Dar es Salaam
na serikali ambayo inataka kuchimba gesi hiyo na baadae kuisaifirisha hadi Dar es Salaam.
Alisema tume hiyo ambayo wajumbe wake watatangazwa baadae, itakuwa na
kazi ya kukutana na wadau wote na baadae kuwasilisha ripoti yake kwake kwa
ajili ya kujadiliwa na Wabunge.
Alisema ripoti ya suala hilo, itajadiliwa na kutolewa uamuzi kabla ya
mkutano wa 10 wa bunge kumalizika.
Aliwataka wananchi wa Mtwara, kutoa ushirikiano kwa tume hiyo ikiwemo
kueleza kwa uwazi kile ambacho wanakipinga ili bunge liweze kujiridhisha.
Wakati
huo huo habari zilizotufikia zinasema serikali imekubali kilio cha wananchi wa
Mtwara wanaotaka gesi inayozaliwasha mkoani humo isisafirishwe kupelekwa Dar es Salaam.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Waziri Mkuu kuongoza jopo
la mawaziri sita kwenda Mtwara kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na mgogoro
huo uliodumu kwa muda mrefu sasa.
Sasa kiwanda cha kuchakata gesi kitajengwa mkoani humo na
karibu megawati 900 za gesi zitakazozalishwa zitabakia mkoani humo, huku
kiwango kidogo cha gesi kikisafirishwa kupelekwa Dar es Salaam.
Serikali imetaja manufaa na faida ambazo wananchi wa
Mtwara wanatarajia kuzipata kupitia mradi huo mkubwa.
Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, George Simbachawene amesema mtambo mkubwa wa kusafishia gesi
utajengwa mkoani humo.
Lakini alisema serikali
pia itajenga viwanda vingine kadhaa, na ujenzi wa mtambo wa megawati 250 ambao
utakuwa ukizalisha umeme na mwingine kujengwa mkoani Lindi eneo la Somanga
Funga utakaokuwa ukizalisha megawati 520.
Akifafanua zaidi
Simbachawene alisema eneo la Mikindani katika kijiji cha Msijute kinatarajiwa
kujengwa kiwanda kikubwa cha saruji Afrika Mashariki na Kati chenye uwezo wa
kutoai ajira kwa watu 6000 jambo ambalo ni manufaa ya Wanamtwara.
Alisema pia tayari kuna
wawekezaji wa viwanda vya mbolea wamejitokeza kujenga viwanda mkoani Mtwara na
serikali itaviacha vinu vya kuchimba na kusindika gesi eneo hilo jambo ambalo
bado ni manufaa makubwa kwa wananchi.
“Viwanda vya kusindika
gesi hii vimepangwa kujengwa maeneo ya Lubasi, Kishere, Mchinga Bay, Lindi,
Sudi Bay, Airport pamoja na Mikindani, viwanda vyote hivi vitatoa ajira kubwa
sana,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa
uzalishaji umeme wa kutosha kwa kutumia gesi utapunguza bei ya umeme na kuuzwa
kati ya senti 6 na 8 za Marekani jambo ambalo litapunguza ugumu wa maisha na
pia bei ya bidhaa nchini.
kwakuwa watanganyika ndio imeundwa tume lkn kama wazanzibari basi wangepelewa wakurya kuwapiga mabomu. amakweli zanziba sinchi.
ReplyDelete