Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, afunga Kikao cha Kumi cha Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akihutubia Baraza la Wawakilishi wakati wa kuahirisha Mkutano wa Kumi,leo jioni hadi mwezi wa April, Kikao hicho kilijadili miswada na kupitishwa na Wajumbe wa Baraza.  

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akinukuu baadhi ya vipengele vya Hutuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa kuahirisha Kikao hicho leo jioni, baada ya kupitisha miswada iliowakilishwa katika Kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza wakifuatilia Hutuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati akiisoma katika mkutano huo wa kuahirisha Kikao cha Kumi cha Baraza leo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia hutuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, akitoka katika Ukumbi wa Mkutano akiwa na Wasaidizi wake, baada ya kuahirishwa kwa Kikao hicho hadi mwezi April mwaka huu. 
 Wajumbe wakisimama wakati Spika akitoka katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza
 Wajumbe wakitoka Ukumbi wa Mkutano.
Wajumbe wakijadili na kubadilisha mawazo wakati wakitoka ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa hadi mwezi April mwaka huu,kutoka kulia Mhe Omar Yussuf Mzee, Mhe. Hamad Masoud Mhe. Juma Duni na Mhe.NassorbMazrui.
Mhe Mohammed Aboud Mohammed Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar  na Said Mbarouk Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wakibadilishana mawazo baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa baraza la Wawakilishi hadi mwezi April mwaka huu. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,aliyoipa mgogo kamera akibadilishana mawazo na Wajumbe wa baraza Omar Ali Shehe na Mbarouk Wadi Mtando, wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.