
Kiungo wa Miembeni FC, Sabri Ally akigombea mpira na kiungo wa Tusker, Justine Monga katika mchezo wa usiku wa jana, Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Miembeni ilifungwa 2-0.

Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Dk. Mwinyihajji Makame Mwadini akisalimiana na mchezaji mkongwe wa Miembeni FC, Monja Liseki kabla ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kiungo wa Miembeni, Issa Othman 'Amasha' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tusker
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
TUSKER FC imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu baada ya kuifunga Miembeni FC ya hapa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa ushindi huo, Tusker itamenyana na Azam katika fainali ya michuano hiyo keshokutwa kwenye Uwanja wa huu huu wa Amaan.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na zote zilishambuliana kwa zamu na kila timu ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga mabao.
Lakini kipindi cha pili Tusker walirekebisha makosa yao na kufanikiwa kupata mabao yaliyowavusha Fainali ya michuano hii.
Bao la kwanza alifunga Luke Ochieng dakika ya 52 kabla ya Jesse Were kufunga la pili dakika ya 72, ambalo linakuwa bao lake la nne katika mashindano haya.
Katika mchezo huo, kikosi cha Miembeni FC kilikuwa; Abdulsamad Sele, Kassim Hamad, Adeyum Saleh, Salum Hajji, Ibrahim Abbas, Sabri Ally, Suleiman Ali/Omar Tamim dk 83, Laurent Mugia/Salim Seif ‘Bakayoko’ dk83, Monja Liseki ‘Anelka’/Peter Ilunda dk 10, Rashid Roshwa/Mohamed Salum dk58 na Issa Othman ‘Amasha’.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Mark Odhiambo, Martin Kizza/Humphrey Okoth dk89, Frederick Onyango, Justine Monga/Andrew Tololwa dk54, Khalid Aucho, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk73, Ismail Dunga na Robert Omonok.
No comments:
Post a Comment