Habari za Punde

Taratibu za Mazishi ya Padri Mushi yakamilika.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Mhashamu Augustino Shayo, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu taratibu za maziko ya Padri Mushi yamekamilika na anatarajiwa kuzikwa kesho katika eneo la Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja 
Amesema Misa ya merehemu Everistitus Mushi itafanyika katika Kanisa Katoliki  Minara Miwili kauzia saa nne asubuhi katika kanisa hilo na kuhudhuriwa na waumini mbalimbali wakati wa misa hiyo.
Pia leo jioni saa kumi itafanyika Ibada ya kumuombea marehemu katika kanisa hilo.
Marehemu Everistitu Mushi ameuawa juzi na watu wasiojulikana katika maeneo ya jirani na Kanisa la Betras wakati akienda kuendesha ibada ya asubuhi kanisani hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.