Habari za Punde

Rais Kikwete Atembelea Majeruhi na Kutowa Mkono wa Pole.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya Hospitali ya  Mount Meru Arusha, kuwatembelea majeruhi wa mripuko wa Bomu katika Kanisa la Olasiti mjini Arusha juzi jumapili .
Rais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu wa hospitali hiyo,alipofika kuwafariji majeruhi akiwana na Mkewe Mama Salma Kikwete. 

Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete, akimfariji mmoja wa majeruhi wa mripoko wa bomu katika kanisa la Olasiti mjini Arusha.

Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete, akimfariji mmoja wa majeruhi wa mripoko wa bomu katika kanisa la Olasiti mjini Arusha.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete , akizungumza na waandishi wa habari kutokana na hali ya maafa ya mlopoko wa bomu katika moja ya kanisa katika mkoa wa Arusha. baada ya kuwatembelea na kutowa mkono wa pole kwa waathirika hao.Picha na Ikulu Dar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.