ABDI SULEIMAN, PEMBA
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuwa haitomvumilia mtu yoyote atakaehatarisha amani na Utulivu wa nchi, itamshughulikia kwa kumchukulia hatua kali za kisheria dhidi yake.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, pia ni Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huko katika uwanja wa michezo wa Skuli ya Chambani wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa jimbo hilo, Mattar Sarahan Said.
Alisema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Dk Ali Mohammed Shein inasema yeyote atakae jaribu kuhatarisha amani na thamani ya nchi ya Zanzibar, haito mvumulia, kwani wazaznibari waliowengi wanahitaji amani ndani ya nchi yao.
Balozi Seif alisema kuwa, pindi nchi itakapoingia katika vurugu kuna uwezekano mkubwa wa kukosekana kwa maendeleo, hata watalii watashindwa kufika Zanzibar kutembelea hali itakayopelekea kukosekana kwa fedha za kimataifa.
“Nchi yoyote duniani iliyokuwa haina amani basi wananchi wake wnaishi kwa shida na wanakosa hata maendeleo, kwani wananchi wa mtwara wamependa hali iliyotokea kwao, ni vizuru tukalinda amani na utulivu wetu wazanzibari”alisema Balozi Seif.
Aidha aliwataka wananchi kuendelea kuishi kwa salama na amani bila ya kubaguana kwa itikadi za chama chochote ili kuweza, kwani amani ikipotea kila kitu kitapotea katika nchi, hivyo wananchi hawana budi kupima yale mambo wanayoambiwa na wanasiasa wasiowatakia mema wazanzibari.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Mattar Sarahan Said, aliwataka wananchi wa chambani kuhakikisha wanampa kura ya ndio ili aweze kuleta historia katika kisiwa cha Pemba, sambamba na kuwaletea maendeleo wananchi wa Chambani.
Matter alisema kuwa pindi wananchi wa chambani watakapo mchagua, atahakikisha wanafunzi wote wanaosoma katika skuli zilizomo ndani ya jimbo hilo, hawatonunua mabuku, Penseli na kalamu kwani vitu hivyo vitatolewa na mbunge.
“Ndugu zangu, dada zangu, kaka zangu na wazazi wangu nawaombeni munipe kura katika uchaguzi ujao, kuwa mbunge wenu wa chambani ili niweze kuwaletea mabadiliko makubwa ikiwemo katika nyanja mbali mbali kama ilani yetu ya CCM inavyoelekeza”alisema Mgombea huyo.
Hata hivyo, aliwataka wananchi wa jimbo la Chambani wasikubali kuhadalika wala kuhadaiwa kimawazo na kiakili kwani, lengo la chama cha Mapinduzi ni kuwaletea wananchi wake maendeleo yaliyokuwa bora.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Wete kupitia viti Maalumu wanawake, Zulfa Abdalla Said, alisema kuwa, lengo lao la kutoka wete kufika Chambani katika kampeni hizo, ni kukipa nguvu chama chao, kwa kudumisha Ummoja wao wanaCCM kutoka wete.
Hata hivyo, alisema kuwa mikakati yake ya kugombea tena kupitia viti maalumu iko pale pele kwa maka 2015 katika jimbo la Wete, ili kuweza kuwa tetea wanawake wenzake pindi atakapopata ridhaa.
Naye mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Chake Chake, Suleiman Abdrahman Juma, aliwataka wanachama wa chama cha Mapinduzi kuhakikiwa wanampigia kura ya ndio Ndugu yao Mattar ili aweza kuwa mkombozi wa wananchi wa Chambani
Hongera, smz, kwakauli nzuri ya kuto mvumilia yoyota atayeleta uchochezi, lakini hata hawa wala nchi wasivumiliwe, wana viangamiza visiwa matumbo nari hawa,kila wizara na idara za serekali wizi, ukuwadi ,ubinapsi na uzembe vimejaa.Hawa muwasho hawasemi kwuwa na jamaa zao wamo, kazi yao eitina,kutugombanisha na ndugu zetu, wa kitanganyika.Wasema wachochezi na wizi wa mali za serekali
ReplyDeleteushajiita mhadim ndugu yangu tutegemee nini kutoka kwako? mungu akuongoze uone mwanga kabla kuingia kaburini
ReplyDelete