Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la wakilishi liwe na tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuiliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wakutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
“Sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuletee ripoti,”alisema Spika.
Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.
Nae waziri wa Nchi afisi ya Makamo wapili wa Rais Muhamed Abuod Mohaamed alisema kuku wanaozalishwa na wanaanchi wa ndani ni tani 163 na nchi inahitaji tani 585 kwa kujitosheleza kimahitaji ,hivyo wazalishaji wa ndani bado uzalishaji wao mdogo.
Waziri huyo alilitaka baraza kuwa, wakiachie kifungu hicho na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar haina ajizi kuwapatia manufaa wananchi wake juu ya suala zima la uzalishaji kuku nchini, na wataliondoa pale uzalishaji wa kutosha ukiwepo.
Ukiendelea mjadala huo waziri wa Afya Juma Duni alisema kumeingizwa kuku bandarini na kamapuni ya Malik Fereji ambao wamezuiliwa kutokana na mmiliki wa kuku hao kuidanganya Serikali kwa kutoa Risiti feki zisizo kuwa za kihalali ,kuibabaisha serikali juu ya kuku hao wanakotoka.
Wazri huyo ameseam kuku hao wazima lakini wataangamizwa na mmiliki huyo atalazimika kulipia gharama za uangamizaji kutokana na kukosa uaminifu.
Nae mwakilishi aliokuwa amezuia kifungu hicho Hamza Hasssa Juma alikubali kukiachia kifungu hicho kwa shingo upande kwa kuilaumu serikali kuwa Bazara la Mapinduzi mapema washapitisha maamuzi kuwasaidia wananchi kuinua zao la kuku lakini wahusika wake bado wamelikalia kimya jambo ambalo halipendezi.
Alisema karibu duniani kote wazalishaji kuku katika nchi hupewa kipau mbele kwa kupewa msukumo wa kifedha ili zao hilo kuzalisha kwa kiwango kikubwa kwa wazalendo na kulimiliki wenyewe wazalishaji wa ndani.
Aidha alisema haitowezekana kontena la futi 20 lililipiwa milioni 30 hapo nyuma na kwasasa kontena la futi 40 kulipiwa milioni nane haiwezekani lazima ichunguzwe.
Mwakilishi aliishauri Serikali kumchukulia hatua za kisheria muingizaji kuku kutoka kampuni ya Malik Fereji kwa kuidanganya serikali kwa hati za uongo kuingizia kuku kutoka nchi sio.
“Inawezekana hata hao waliopita walingizwa kwa njia hiyo hiyo”alisema Hamza.
Hata hivyo alimuomba Spika ampe uhuru wa kuunda tume itayo weza kujitegemea wenyewe kulifuatilia suala zima la kuku hapa Nchini na nje ya Nchi kulifuatilia, na bila ajizi spika alikubali kuunda tume hiyo na kutakiwa kutafuta wezake wakufuatilia jambo hilo.
No comments:
Post a Comment