Habari za Punde

Wagomea Mazishi Wakidai Marehemu alikuwa na VVU.

Na Masanja Mabula, Pemba
BAADHI wananchi wa Shehia ya Ukunjwi Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wamegomea mazishi ya marehemu aliyekuwa anaishi ya VVU.

Taarifa ambazo zimepatikana na mwandishi wa habari hizi zinasema kuwa mazishi hayo ya marehemu Fatma Suleiman Ngasa (Chausiku) yalichelewa kufanyika kutokana na wananchi kutofautiana na kila upande ukisusa kutokana na kuhofu kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Chanzo chetu cha habari kinasema wanachama wa ZAPHA+ Wilaya ya Wete walilazimika kuchukua gari kwenda kumstiri mwenzao, baada ya kupata taarifa kwamba wananchi wa Shehia hiyo wameendesha mgomo baridi .

Aidha chenzo chetu kimezidi kufahamisha hata suala la dini nalo lilichukua nafasi yake, licha ya marehemu huyo kuwa ni muumini wa dini ya Kiislamu, lakini baadhi ya wananchi walionekana kupingana na maelezo yaliyotolewa na ndugu wa marehemu.

"Unajua bado jamii inashindwa kuelewa njia za maambukizi, hali hiyo ndiyo iliyopelekea kuchelewa kufanyika kwa mazishi wa marehemu , lakini tunashukuru sana uongozi wa Sheha kwa kulisimamia hadi mazishi kufanyika, " kilifahamisha chanzo chetu cha habari .

Aidha habari za uhakika ambazo zimepatikana na mwandishi wa habari hizi zinasema msukumo wa kufanyika kwa mazishi hayo pia ulichangiwa na wanachama wa ZAPHA+ ambao walishirikiana na sheha kuona mwili wa marehemu unahifadhiwa katika makaazi yake ya kudumu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Sheha wa Shehia ya Ukunjwi, Mkongwe Kasanje amesema hali ya mabishano iliyokuwepo wakati wa mazishi wa hayo iliepelekea kuchelewa kwa muda shughuli za kuustiri mwili wa marehemu.

Sheha huyo aliishangaa jamii kuona inashindwa kutambua njia za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi , licha ya elimu ya Ukimwi kuendelea kutolewa siku hadi siku.

" Mimi naamini jamii jamii imeshapata elimu ya Ukimwi , lakini hii imenipa wasi wasi wa kwamba bado elimu zaidi inahitaji kutolewa ili jamii iweze kutambua kwamba unyanyapaa wa watu wanaoishi na VVU hauna nafasi katika jamii ya leo," alifahamisha.



4 comments:

  1. Mimi si-ilaumu jamaii kutoa jua nini maana ya Kumsaidia Mgonjwa wa Ukimwi tu bali hata kumzika.

    Isipokua nailamu Serikali ya SMZ- inayoongozwa na Chuki za Ki-CCM, Upemba. Kushindwa kuelimisha jamii za watu wa Pemba kwa njia za Redio na TVZ. Nikisema hivyo nimaana kwamba Pemba hakuna Mitambo ya Redio wala TV.

    Na hiyo Mibovu iliowekwa Marchine zake zilingolewa na Waziri Kiongozi wa awamu ya 7 Shamsi Vuai Nahodha nakzichukua katika Mtambo wa Unguja kama vile Pemba hawana haki.

    Visiwa Wamedumazwa kwa Sisa tu kila ukisikia RRedio inatangaza kitu au Kuonyesha activities (.kwa uande wa Pemba..) ni Ziara za Raisi, UVCCM, mikutano ya CUF. Hushangaa kwanini Redioo zetu, magazeti, na TVzinaonyesha matokeo ya iongozi na Siasa tuu.

    Ndio tuseme hakuna mambo mengine ya maendeleo ambayo yanaweza kutolea na Redio, magazetui au Tv. na hili ndilo linalowasumbua watu wa Visiwani kushindwa kua Creative. kwasababu hawana Vielelezo vya Mifano ya mambo mengine ya Maendeleo isipokua CCM, Mkutano, CUF, Mkutano au Raisi na Mwenge n.k

    ReplyDelete
  2. dawa ya mambo yote haya ni kuhakikisha katika masuala ya katiba wananchi tujitokeze kwa wingi kudai nchi yetu ya zanzibar iwe huru kutokana na muungano , hizi fitna zote zitaondoka tukijitawala bila muungano , tatizo SMZ ni serikali kibaraka hutekeleza yale ambayo yanafaida na serikali ya muungano

    ReplyDelete
  3. Maoni mazuri lkn. jazba imezidi kiasi kiasi kwamba hata maneno mengi yamekosewa!

    Tutumieni busara jamani, huenda viongozi wakatuelewa!

    ReplyDelete
  4. Kwani huu muungono ndio uloleta ukikimwi, swala hapojuu watuku nyanya paa maiti kwa kuwa kafa ukwimwi lakini waleo wanya hivyo hawajijui wao watakufa vipi?,wali lakudai nchi haliku taja hapo au ndi mnataka kujionesha kuwa mua msho mnaugonja,sasawenzenu wametulia wana tuacha tufunge ramadhan hakuna kuwa umeonekachina wala japani sete sikumoja

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.