Habari za Punde

Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi yaangamiza bidhaa zisizofaa

 Bodi ya madawa inafanya kazi zake kwa uadilifu mana dawa hizi zinazoangamizwa zilikua zishamaliza muda wake wa matumizi tangu mwezi wa sita lakini bado zilikua zikiuzwa kwenye pharmacy zetu

 Mchele mbovu tani 40 umeangamizwa leo na Bodi ya madawa, chakula na vipodozi Zanzibar( ZFDB) katika eneo la Kibele.
 Shehena ya Vyakula vibovu na dawa vikitolewa katika ofisi za Bodi ya Chakula, dawa na vipodozi tayari kwenda kuangamizwa.
 Tende iliyoingizwa Zanzibar ikiwa ishamaliza muda wake wa matumizi yaangamizwa.

Wale warembo kuweni makini na vipodozi vyenye sumu. Bodi ya dawa,chakula na vipodozi ikiangamiza vipodozi vyenye sumu.Jamani tuwe makini na dawa hizi zilizokua hazina viwango kwa matumizi ya Binadamu.
Picha zote na Haroub Hussein

1 comment:

  1. Hii ni khatwa lakini haitoshi kuteketeza bali inafaa na hao wamiliki iwapo walikuwa bado wanaziuza bidhaa hizo wapelekwe mahakamani na ikiwezekana wanyanganywe leseni za kufanyia biashara na kusiwe na muhali kwa kuhatarisha afya na Kaisha ya binadamu.Vile vike inafaa kuangalia uwezekano wa kuvitumia hivyo vyakula kwa njia nyengine kama malisho ya mifugo badala ya kuviteketeza

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.