Habari za Punde

Mungu wa Mabaniani Bado Kupatikana.

Sanamu la Mungu wa Kibadiani lililoibiwa miezi mitatu iliopita ndani ya jingo la Ibada la Madhehebu ya Hindi yaliopo katika mtaa wa Kiponda Mjini Unguja , bado hadi sasa hakupatikana licha ya juhudi za kumtafuta zikiendelea .

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Jumuiya ya Hindu Zanzibar (Hindu Union) wameweka zawadi nono kwa mtu atakaefanikisha kupatikana kwa Mungu huyo atapata zawadi hiyo.
  
Mungu huyo mwenye umbo la Kibinaadamu anayejulikana kwa jina la Rabi Chrisma anayevalishwa nguo mpya kila siku asubuhi, alitengenezwa kwa madini ya shaba na kukisiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani  2000/= aliibiwa miezi mitatu iliopita katika mazingira ya kutatanisha.

Hadi hivi sasa hakujapatikana habari yoyote kuhusiana na kupatikana kwa Mungu huyo, licha ya Waumini wa madhehebu hayo kuwa na wakati mgumu wakiwa katika ibada zao kutokana na Mungu huyo kuibiwa.

Hivyo nafasi ya Mungu huyo aliyeibiwa hivi sasa imezibwa kwa kuwekwa picha inayofanana nae ili waumini hao waweze kuendelea na ibada zao hadi hapo Mungu mwengine atakapotengenezwa au kupatikana aliyeibiwa.


Ile siku aliyoibiwa tulishindwa kufanya ibada kwa sababu Mungu hayupo, lakini hivi sasa tumeamua kuweka picha kama yake ili ibada zisisite ziendelee kama kawaida hadi atakapotengenezwa Mungu mwengine
alisema, Bhagwansim Meisura Mjumbe wa Wahindu Zanzibar.
Akizungumzia tukio la kuibiwa kwa Mungu huyo Bhagwansim alisema ameibiwa katika mazingira ya kuktatanisha wakati jengo likiwa limekuvunjwa.

Alidai tukio hilo linamtuhumu sana mlinzi ambae alikataa kuhusika na wizi huo, baada ya kuhojiwa alipofikishwa katika vyombo vya kisheria.kwa upelelezi 
Hata hivyo mlinzi huyo alidai alirejea kwao Tanzania bara baada ya kuachwa kazi ndani ya jengo hilo ambalo pia linakaliwa na Sharifu Mkuu kutoka Bombay ambae shughuli zake kubwa ni kuendesha ibada ndani ya jengo hilo pamoja na mambo mengine yanayohusiana na dini hiyo.
Kutokana na wizi huo, Uongozi wa Umoja wa Hindu Zanzibar hivi sasa umo mbioni kutafuta sanamu nyegine ili iwe kama Mungu wa kumuabudia na waweze kuendesha ibada zao kama alivyokuwa hapo awali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Khamis Mkadam, kwa upande wake amesema kuwa Polisi bado haijapata taarifa zozote kuhusiana na wizi huo wa Mungu wao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.