Habari za Punde

Update : Ajali ya Mv Kilimanjaro

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Dk Khalid akizingumza na waandishi wa habari usiku huu.
 
Picha kutoka Facebook

Taarifa zilizopatikana ni kwamba boti ya Azam Marine, Mv Kilimanjaro imefanikiwa kuwasili Bandari ya Malindi licha ya kukumbwa na dhoruba kali eneo la Nungwi, dhoruba iliyopelekea baadhi ya mizigo kupunguzwa na mengine kuanguka baharini baada ya eneo la mbele ya Boti hiyo kuingiwa na maji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya usafiri baharini.
 
 
Maiti wote wameletwa mjini kwa ajili ya kutambuliwa wapo katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Serikali itaandaa utaratibu wa kawaida kwa maiti hizi kuzikwa ama kupewa jamaa zao.

Kepteni Nassor Abubakar Khamis ameshikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano.
Jumla ya abiria 396 walikuwemo katika manifesto ya safari hii kutoka Pemba kulekea Unguja.

Zoezi la kutafuta miili ya walioanguka baharini litaendelea kesho asubuhi baada ya kusitishwa kwa kuingia kiza.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.